Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari Jerry Silaa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha
……….
Happy Lazaro, Arusha .
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari Jerry Silaa amewataka watanzania kutoa taarifa za Utapeli Polisi pindi inapojitokeza katika mitandao ya Simu kwa lengo la kukomesha vitendo vya wizi wa mitandao nchini.
Waziri Silaa ameyasema hayo leo mkoani Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano wake na wanahabari wa kutolea ufafanuzi wa Uzinduzi wa Kampeni ya Sitapeliki uliofanyika ofisi za Makao makuu ya Umoja wa Posta nchini Zilizopo Arusha.
Aidha amewataka kutambua kuwa hakuna pesa za bure zinazoweza kutolewa katika Mitandao ya Simu hivyo asilimia kubwa ya utapeli unaofanyika ni pamoja na jumbe zinazotumwa kwanjia ya linki (mwunganiko) ambazo wananchi wengine wamekuwa wakifungua na kufuata maelekezo ambapo mwisho wa safari wanahitimisha na kilio cha kutapeliwa.
Waziri Slaa amewataka wananchi kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha pindi wanapokutana na changamoto mbalimbali ikiwemo kutoweka namba za siri ambazo zinakuwa rahisi kwa matapeli hao kuzigundua na kuweza kufanya utapeli kwa urahisi.
Wakitoa maoni yao katika Mkutano huo baadhi ya waandishi wa Habari wameshauri kampuni za Simu kutoa huduma kwa haraka pindi wanapotafutwa na watumiaji wa Simu au mitandao ili kurahisisha utoaji wa taarifa na kuendelea kuimarisha huduma nzuri na za haraka kwa wananchi.
Mkutano wa Waziri wa Mawasiliano na teknolojia ya habari umekuja siku moja mara baada ya kuzinduliwa kwa kampeni ya “Sitapeliki” iliyofanyika mkoani Arusha katika Kikao kazi cha Serikali na wadau wa sekta ya mawasiliano na teknolojia ya habari kuhusu utekelezaji wa mkakati wa taifa wa uchumi wa kidigital 2024 /3034.