Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akisaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Bw. Johnson Nkondo aliyekuwa
Msaidizi wa Ofisi Mkuu – Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kuwasili katika
makazi ya familia eneo la Veyula mkoani Dodoma leo tarehe 16 Februari 2025.
(Pembeni ni mwenza wa Makamu wa Rais Mama Mbonimapaye Mpango)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na
mwenza wake Mama Mbonimapaye Mpango wakimfariji Bi.Mwajuma Mnyandwa
ambaye ni mjane wa marehemu Johnson Nkondo aliyekuwa Msaidizi wa Ofisi Mkuu –
Ofisi ya Makamu wa Rais wakati walipowasili makazi ya familia hiyo Veyula Mkoani
Dodoma leo tarehe 16 Februari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akiwafariji waombolezaji mbalimbali wakati alipowasili katika makazi ya familia ya
aliyekuwa Msaidizi wa Ofisi Mkuu – Ofisi ya Makamu wa Rais, marehemu Johnson
Nkondo leo tarehe 16 Februari 2025 Veyula – Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Msaidizi wa Ofisi Mkuu – Ofisi ya
Makamu wa Rais, marehemu Johnson Nkondo alipowasili katika makazi ya familia
hiyo Veyula Mkoani Dodoma leo tarehe 16 Februari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akizungumza na waombolezaji waliojitokeza katika makazi ya familia ya aliyekuwa
Msaidizi wa Ofisi Mkuu – Ofisi ya Makamu wa Rais, marehemu Johnson Nkondo
Veyula Mkoani Dodoma leo tarehe 16 Februari 2025.
……………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na
mwenza wake Mama Mbonimapaye Mpango wameifariji familia na waombolezaji
mbalimbali kufuatia kifo cha Bw. Johnson Nkondo aliyekuwa Msaidizi wa Ofisi Mkuu –
Ofisi ya Makamu wa Rais aliyefariki tarehe 13 Februari 2025 katika Hospitali ya
Benjamini Mkapa mkoani Dodoma wakati akipatiwa matibabu.
Makamu wa Rais na Mwenza wake wametoa faraja hizo walipowasili katika makazi
ya familia ya Marehemu Johnson Nkondo eneo la Veyula mkoani Dodoma leo tarehe
16 Februari 2025.
Akizungumza na waombolezaji, Makamu wa Rais amesema marehemu Nkondo
alikuwa muadilifu aliyezingatia maadili ya utumishi wa umma na taratibu za kiofisi
wakati wote wa utumishi wake.
Amesema ni vema kumuenzi marehemu Nkondo kwa
kujifunza namna alivyojitolea kulitumikia Taifa kwa uadilifu mkubwa pamoja na
kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake vema, kuishi vema na ndugu,
majirani na marafiki.
Makamu wa Rais amewaombea faraja ya Mwenyezi Mungu iwafikie familia, ndugu,
jamaa na marafiki walioguswa na msiba huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule aliyeshiriki katika msiba huo,
ametoa pole kwa familia na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kumpoteza mtumishi
hodari. Amewasihi familia na waombolezaji kuendelea kumuomba Mungu awavushe
salama katika kipindi kigumu cha msiba huo.
Marehemu Johnson Nkondo alizaliwa tarehe 20 Aprili 1966 na anatarajiwa kuzikwa
tarehe 17 Februari 2025 kijijini kwao Bombo Wilaya Same mkoani Kilimanjaro.