Beki wa Arsenal, Hector Bellerin (kulia) akishangilia na Granit Xhaka baada ya kuifungia timu hiyo bao la kusawazisha zikiwa zimesalia dakika tatu katika sare ya 2-2 na wenyeji, Chelsea usiku wa jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London. Bao lingine la Arsenal iliyomaliza pungufu baada ya beki wake wa kati, David Luiz kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea rafu Tammy Abraham kwenye boksi lilifungwa na Gabriel Martinelli dakika ya 63, wakati ya Chelsea yalifungwa na Jorginho kwa penalti dakika ya 28 na Cesar Azpilicueta dakika ya 84 PICHA ZAIDI SOMA HAPA
ARSENAL WALIOCHEZA PUNGUFU WAICHOMOLEA CHELSEA 2-2 DARAJANI
By Alex Sonna
January 22, 2020 | 11:30 am

Related Stories
View all
Michezo
2 days ago
SIMBA SC YAENDELEZA UBABE LIGI KUU, YAICHAPA JKT TANZANIA
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliopigwa…
Michezo
2 days ago
MUHAS YAHAMASISHA JAMII KUJALI AFYA KUPITIA MAZOEZI
Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Bruno Sunguya, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof. Appolinary Kamuhabwa, pamoja na…
