Happy Lazaro , Arusha .
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Philip Mpango ametoa rai kwa mamlaka ya serikali mtandao (e-GA) kukamilisha mchakato wa kusanifu na kujenga mfumo mkuu wa ubadilishanaji taarifa serikalini.na kuhakikisha taasisi zote za umma zinajumuishwa katika mfumo huo.
Ameyasema hayo.leo mkoani Arusha wakati akifungua kikao kazi cha tano cha mamlaka ya serikali.mtandao kinachofanyika mkoani Arusha .
Dkt Mpango amesema jambo hilo.ni muhimu ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi kama ilivyoelekezwa na Rais wa Tanzania Dkt.Samia.Suluhu Hassan kwa taasisi za umma kuhakikisha kuwa mifumo yao inasomana na kubadilishana taarifa.
Aidha Makamu.wa.Rais amesema taasisi zote za umma zinapaswa kushirikiana na mamlaka ya serikali mtandao katika hatua zote za ujenzi au ununuzi ,usimamizi na uendeshaji wa kiradi ya TEHAMA pamoja na kuwataka kuwaelekeza wakuu wote wa taasisi za umma kuzingatia Sheria kanuni.na miongozo inayotolewa na mamlaka husika katika utekelezaji wa shughuli za serikali mtandao.
Kwa upande wake Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora , George Simbachawene amesema kuwa e-GA ni kiunganishi cha kupeleka huduma kwa wananchi kwa urahisi ili wananchi wapate huduma stahiki kwa haraka bila kuwepo kwa vitendo vya rushwa.
“Dunia ya leo e-GA ni kama muundo wa kurahisisha mifumo ndani ya serikali na utoaji huduma kwa urahisi katika mifumo ya serikali ,niwapongeze kwa hatua na malengo haya na mimi.kama kiongozi naridhika kuwa e-GA mmefanya kazi yenu sawasawa.” amesema Simbachawene.
Ameongeza kuwa lengo la kuandaa kikao kazi hicho ni kiwakutanisha wadau wa serikali mtandao katika.taasisi na mashirika ya umma na sekta binafsi ili kuwapatia fursa ya kujadili hatua iliyofikia katika utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao.
Naye Mkurugenzi mkuu wa e-GA ,Mhandisi Benedict Ndomba amewashukuru washiriki wote kwa kuweza kufika kwani mkutano huo utaleta tija kwao katika utendaji kazi wa kila.siku pamoja na kufanya maboresho ya mifumo ya e-GA.
Nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo ,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya wazawa inayojihusisha na utoaji wa mafunzo kwa wataalamu wa TEHAMA na watoaji wa ushauri katika mambo ya usalama mtandaoni (digital public infrastructure (DPI) ,Upendo John Kimbe amesema kuwa ,kampuni hiyo inasaidia serikali katika kufikia malengo ya utoaji huduma mbalimbali kwa wananchi kupitia serikali mtandao.
“Tumekuja katika.kongamano hili kwa lengo la kuisaidia serikali katika kutoa huduma kwa wananchi wake kw hiyo katika hili tumekuja katika eneo hilo la digital Tanzania kusaidia na kuona ni jinsi gani Cybergen inaweza ikachangia katika mchakato mzima wa kuifanya Tanzania kuwa ya kidigitali. “amesema.
Upendo ameongeza kuwa, wamekuwa wakijihusisha na utoaji wa mafunzo ya ICT ambazo ni kozi za kitaalamu katika upande wa IT ambazo ni miongoni mwa huduma wanazozitoa ambapo wana uwezo wa kutoa huduma zote kwani wakufunzi wao wanatokea nchi mbalimbali duniani ili kuweza kuleta ujuzi wao haoa nchini .
“Katika kufanya Tanzania kuwa ya kidigitali tumeweza kuwajengea uwezo watalaamu wetu wa ndani na sio kutegemea wataalamu kutoka nje kwani ni lazima kuwajengea uwezo watu wetu wa ndani ili kuwa na Tanzania tunayoitaka.”amesema Upendo.
“Sisi kuwepo hapa tunawafanya wataalamu.mbalimbali waweze kututambua kuwa kuna kampuni ya kitanzania ina uwezo wa kuleta wataalamu kutoka nje ya nchi ikiwemo Ulaya,India na Marekani.”ameongeza.



