NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Wenyeji Simba Sc wamefanikiwa kuibaka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara uliochezwa leo Katika Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na viungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 29, Mkongo Ellie Mpanzu Kibisawala dakika ya 44 na mzawa Ladack Juma Chasambi dakika ya 45 + 2.
Kwa ushindi huo, Simba Sc inafikisha pointi 47 na kurejea kileleni mwa ligi kuu ikiwazidi pointi moja mabigwa watetezi Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 18.
Kwa upande wao Tanzania Prisons baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi 17 za mechi 18 na kushika nafasi ya 14 katika ligi yenye timu 16.