Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis akichangia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa mwaka 2024
iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma leo Februari 05, 2025.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria
Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za
kamati hiyo kwa mwaka 2024 bungeni jijini Dodoma leo Februari 05, 2025.
…………
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Khamis amewaomba Watanzania kuendelea kuuenzi na kuudumisha
Muungano kwani umeleta manufaa makubwa.
Amesema hayo wakati akichangia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kamati
ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa mwaka 2024
iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma leo Februari 05, 2025 na Mwenyekiti wa
kamati hiyo Mhe. Dkt. Joseph Mhagama.
“Muungano wetu ndio utaifa wetu tuendelee kuenzi Muungano wetu kwa
maslahi mapana ya vizazi vijavyo na vinavyokuja,” amesisitiza Mhe. Khamis
huku akiongeza kuwa Muungano huu ni wa kipekee ukilinganisha na nchi
zingine duniani zilizoungana lakini Muungano wao haukudumu.
Amesema kuwa hatuna budi kuwashukuru na kuwapongeza Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali
Mwinyi kwani kwa busara zao wamefanya kazi kubwa ya kuusimamia na
kuulinda ambapo hivi Aprili 26, 2025 unatarajia kutimiza miaka 61 tangu
kuasisiwa kwake.
Akiendelea kuchangia taarifa hiyo, ameongeza kuwa uwepo wa Kamati ya
Pamoja imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha linapotokea jambo la mgongano,
kamati hiyo inakutana kwa kwa pande zote mbili kwa lengo la kuhakikisha
inatatua na Muungano unaendelea kuwa salama.
Amesema viongozi hao wakuu kupitia Serikali zote mbili wamefanya kazi
kubwa na kuwazesha kupatiwa ufumbuzi wa changamoto za Muungano Zaidi
ya 15 na kuufanya uendelee kudumu.
Kuhusu hoja ya uwepo wa Ofisi za Muungano kwa upande wa Zanzibar, Mhe.
Khamis amefafanua kuwa zipo Taasisi 33 zinazohusa Muungano na tayari 21
zina majengo ambayo yana ofisi zake.
Awali akiwasilisha taarifa hiyo, Mhe. Dkt. Mhagama amesema Bunge
limeazimia Serikali ihakikishe ihakikishe ujenzi wa ofisi na majengo ya kudumu
kwa upande wa Zanzibar ili kurahisisha utoaji wa wahuduma kwa wananchi.
Hivyo, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepokea na kukubali
taarifa ya shughuli za Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria Miundombinu kwa
mwaka 2024 iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma leo Februari 05, 2025.