Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Kijana mnufaika wa mafunzo ya ufundi stadi VETA ambaye ni mlemavu Ndugu Abdi Athumani Kipara kuhusu kazi yake ya ushonaji wa mabegi mara baada ya kutembelea banda la maonesho la VETA nje ya ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea tuzo Maalum kuhusu maono na mchango wake kwenye sekta ya Elimu kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolph Mkenda wakati wa hafla ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2025