Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Paul Matiku Chacha mfano wa ufunguo wa magari kwa ajili ya huduma ya afya inayotembea (Mobile Clinic) kwa Wilaya ya Sikonge na Uyui yaliyotolewa na Jakaya Kikwete Foundation chini ya ufadhili wa Kampuni ya SC Johnson Family ya Marekani, leo tarehe 1 Februari, 2025, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiangalia mfano wa majengo ya vituo vya afya kwa ajili ya huduma za mama na mtoto yatayojengwa na Jakaya Kikwete Foundation chini ya ufadhili wa Kampuni ya SC Johnson Family ya Marekani katika mikoa ya Kagera, Katavi, Kigoma, Mwanza na Rukwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa kampuni ya SC Johnson Family Dkt. Fisk Johnson kutoka Marekani pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma leo tarehe 1 Februari, 2025.