Akikabidhi misaada hiyo kaimu meneja wa TRA mkoa wa Njombe Beatrice Kahoho amesema huo ni muendelezo wa kurejesha fadhira kwa jamii katika wiki ya shukrani kwa mlipa Kodi ili iwasaidie wanafunzi hao wenye mahitaji Maalumu kujikimu.
Mkuu wa shule ya Sekondari Viwizi Mwalimu ameshukuru kwa msaada huo na kwamba Kumekuwa na changamoto kubwa ya mahitaji kwa wanafunzi hao ambao wanatoka familia zenye Uwezo tofauti.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi hao akiwemo Abigael Lawi wamesema misaada hiyo itakwenda kuwasaidia kupunguza baadhi ya mahitaji hususani kwa watoto wa kike ambao wamepata Taulo za kike pia
TRA inatarajia kuhitimisha Wiki ya Shukrani kwa mlipa Kodi hapo Februari Tano Mwaka huu kwa kutoa tuzo mbalimbali kwa wadau na wafanyabiashara waliofanya vyema kwenye sekta ya Kodi.