Rais wa serikali ya wanafunzi chuo.cha ufundi Arusha,Haruna Banana akizungumza kuhusiana na application hiyo chuoni hapo
Aliyepo kulia ni Mmojawapo wa waanzilishi wa application hiyo Dk Raza Roshan akiwa na mwanzilishi mwenzake ,Ahmed Raza wakati wakizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha.
…………
Happy Lazaro,Arusha .
Kampuni ya teknolojia ya HEALTH IQ inayojihusisha na swala la Afya ambayo hutumia akili bandia imeanzisha application ya Health IQ kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa afya .
Akizungumza wakati wa kutambulisha application hiyo mpya kwa wanafunzi wa chuo cha ufundi Arusha ,Waanzilishi wa application hiyo ,Dk Raza Roshan na Ahmed Raza wamesema kuwa ,application hiyo ni nzuri sana na inasaidia kila siku kwani unapata meseji inayokupa taarifa ya maswala la Afya .
Wamesema kuwa, application hiyo ni kama zawadi kwani hii ni awamu ya kwanza kwa mkoa wa Arusha na wataendelea na mchakato huo katika vyuo mbalimbali kwani huu ni mwanzo tu .
Ahmed Raza amesema kuwa, application hiyo ina manufaa matatu ambayo ni pamoja na kufanya ufuatiliaji wa afya ya akili na kumwezesha mtu kupata utulivu wa akili .
Ameongeza kuwa,application hiyo inaripoti mambo manne ya afya ambayo ni nje ya afya ,ndani ya afya ,kiakili na kijamii kwani kikubwa wanachofanya ni uchunguzi wa afya .
Amewataka wananchi wa Arusha kuitumia application hiyo kwani ina manufaa makubwa na haina gharama yoyote na inaweza kukuwezesha kufuatilia mwenendo wa afya yako kwa ujumla.
“Tumechagua chuo hiki kwani Kuna watu wanaona kitu kipya na kuhoji, wanakipinga. na hatimaye kukubali,wanaitwa Wafuasi… halafu kuna watu wanaona teknolojia mpya, kitu kipya, na wanaikubali na kuithamini… wanaitwa viongozi, tulichagua Arusha Technical kwa sababu walikuwa viongozi na mstari wa mbele katika mapinduzi haya ya Afya!”amesema .
Kwa upande wake Rais wa serikali ya wanafunzi chuo cha ufundi Arusha ,Haruna Banana amesema kuwa, kuletwa kwa application hiyo chuoni hapo inasaidia sana kwani matumizi ya akili bandia na kada ya afya zinaenda pamoja kwani zinagusa wanafunzi wanaosoma kozi hizo .
“Applicationa hii ni kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa afya kwani inachukua fursa kwao kuweza kujifunza na kufahamu afya zao na imeanzia hapa chuoni kwani ndipo kuna watumiaji wakubwa wa simu kubwa na application hiyo inagusa wale ambao wanashughulika na maswala ya kiafya na kimtandao”amesema .
Amesema kuwa, application hiyo ni kama.zawadi kwao hivyo amewashauri serikali.ya wanafunzi wa chuo hicho kuhakikisha wanakuwa na application hiyo kwenye simu zao.
Hata hivyo ameshukuru kampuni hiyo kwa kuja na application hiyo kwani inasaidia sana kuweza kufuatilia mwenendo wa afya zao na kuweza kuchukua tahadhari ya haraka kuhusu maswala ya afya kwa ujumla.