Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pemne Juma amesema uanzishwaji wa Majikwaa ya uwezehaji wanawake kiuchumi katika shehia, kutasaidia kuwafikishia fursa mbali mbali wanawake na kwa wakati.
Mhe Riziki ameyasema hayo wakati alipofungua mafunzo ya Uanzishwaji wa Majukwaa ya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kwa Masheha na Waratibu wa Mkoa wa Kusini Pemba, yaliyofanyika katika ukumbi wa …Mkoani Pemba.
Amesema lengo la kuanzishwa majukwaa hayo ni kutekeleza maagizo ya viongozi wa nchi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika kuhakikisha fursa zinazotolewa zinawafikia walengwa.
Amefahamisha kuwa sifa ya kuwepo majukwaa ndani ya shehia ni kuhakikisha kunakuwa na vikundi vilivyosajiliwa, hivyo ametoa wito kwa masheha kuhakikisha wanavisaidia vikundi vilivyomo kwenye shehia zao ili kuweza kusajiliwa na kuweza kuingia kwenye majukwaa.
Hata hivyo amewaomba Masheha na Waratibu baada ya kuundwa majukwaa hayo kuhakikisha wanachagua viongozi watakaosimamia majukwaa yao ambao wanatoka ndani ya shehia zao ili kuona fursa zitakazotolewa zinawafikia wahusika, na wasikubali kupandikiziwa watu ambao hawamo ndani ya Shehia zao.
Wakitoa michango yao katika mafunzo hayo, baadhi ya Waratibu na Masheha wamesema watajitahidi kuwaelimisha jami iliyowazunguka kuhusu uanzishwaji wa majukwaa pamoja na kuwahamasisha kujiunga katika vikundi na kuvisajili ili waweze kufaidika na fursa zitakazotolewa ma viongozi wao.