Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally Chirukile wakati akimkabidhi mjasiliamali jiko la gesi
Baadhi ya wajasiliamali waliopatiwa majiko ya gesi ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia
………………..
Neema Mtuka Sumbawanga
Rukwa:Wajasiriamali zaidi ya 200 wanaouza Chakula katika Soko la Mandela Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa wamekabidhiwa majiko ya gesi yatakayowawezesha kufanya shughuli zao kwa urahisi.
Majiko hayo yamekabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally Chirukile kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia_Suluhu_Hassan ikiwa na lengo la kuhamasisha Wajasiriamali hao kutumia nishati safi.
Zoezi hilo limefanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela lilipokuwa likifanyika Bonanza la Kumbukizi ya kuzaliwa Rais Samia likishuhudiwa na viongozi mbalimbali na mamia ya wakazi wa Mkoa wa Rukwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wajasiriamali hao wamemshukuru Rais Samia kwa kuwapatia majiko hayo huku wakieleza hisia zao chanya juu yake na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa matumizi ya nishati safi.
Nao baadhi ya wananchi akiwemo sarafina Mizengo amesema elimu ya upandaji miti kwa lengo la utunzaji wa mazingira itolewe ili wananchi wawe na uelewa wa kutosha.
“Ni muhimu wananchi wakapewa elimu ya kutosha juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia na namna bora ya kutunza miti .