Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme wakati akifungua Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi kuhusu Hifadhi ya Mazingira Januari 27, 2025 jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkataba wa Nairobi kuhusu Hifadhi ya Mazingira Dkt. Jared Bosire (wa pili kulia) akizungumza wakati wa Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi kuhusu Hifadhi ya Mazingira Januari 27, 2025 jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme, kuanzia kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi. Farhat Ali Mbarouk na Afisa Kiungo wa Mkataba wa Nairobi Bw. Wankyo Mkono.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme wakati akiwa na Afisa Kiungo wa Mkataba wa Nairobi Bw. Wankyo Mkono wakati wa Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi kuhusu Hifadhi ya Mazingira Januari 27, 2025 jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme wakati akisalimiana na Mkuu wa Mkataba wa Nairobi kuhusu Hifadhi ya Mazingira Dkt. Jared Bosire wakati wa Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi kuhusu Hifadhi ya Mazingira Januari 27, 2025 jijini Dar es Salaam. Katikati ni Afisa Kiungo wa Mkataba wa Nairobi Bw. Wankyo Mkono.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi kuhusu Hifadhi ya Mazingira Januari 27, 2025 jijini Dar es Salaam. Katikati ni Afisa Kiungo wa Mkataba wa Nairobi Bw. Wankyo Mkono.
……….
Nchi za Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi zimetakiwa kushirikiana katika kulinda mfumo ikolojia inayotegemea afya ya bahari na ukanda wa pwani.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme wakati akifungua Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi kuhusu Hifadhi ya Mazingira Januari 27, 2025 jijini Dar es Salaam.
Amesema Mkutano huo unaoshirikisha nchi wananchama ambazo ni Comoro, Kenya, Somalia, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, Shelisheli, Re-Union, Afrika Kusini na Tanzania unaashiria hatua kubwa ya maendeleo katika kuhakikisha ulinzi na matumizi endelevu ya rasilimali za Bahari ya Hindi.
Bi. Mndeme ameeleza kuwa Tanzania inajivunia kuwa Mwenyekiti wa Mkataba wa Nairobi na imetoa kikamilifu katika kuendeleza malengo na madhumuni ya mkataba huu kwa manufaa ya mazingira ya bahari katika Ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi (WIO).
Ameahidi kuwa Sekretarieti ya Mkataba wa Nairobi kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) itaendelea kufanya kazi pamoja na Sekretarieti ya Mkataba wa Nairobi katika kufikia mafanikio yaliyolengwa yaliyooneshwa katika Mpango wa Kazi (2025-2028) na Maamuzi ya COP 11.
Aidha, Bi. Mndeme amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake thabiti ya kuhifadhi mazingira ya baharini na kuendelea kuunga mkono katika utekelezaji wa programu ya kazi na Maamuzi ya COP 11.
“Chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia tunapiga hatua kubwa katika ulinzi wa mazingira, hasa kupitia uhamasishaji wa vyanzo vya nishati safi na endelevu,” amesema Naibu Katibu Mkuu Mndeme.
Mkutano huo unaotarajiwa kufungwa Januari 31, 2025 umewakutanisha wataalmu kutoka SJMT na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) maafisa viungo wa kitaifa, mashirika na taasisi za kitafiti.