Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza Michael Lushinge (kulia) akisalimiana na baadhi ya viongozi.

Viongozi wakifuatilia matukio mbalimbali katika mkutano wa kumpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais .

Baadhi ya wakazi wa Mwanza wakiwa kwenye viwanja vya ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano 

…………….. 

Hellen Mtereko,Mwanza

Makundi mbalimbali yamejitokeza katika viwanja vya Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza kwaajili ya kuunga mkono maazimio ya Mkutano mkuu ya kumchagua Dkt.Samia Suluhu kuwa mgombea urais wa Tanzania Bara na Dkt.Nchimbi kuwa mgombea mwenza.
Makundi hayo wakiwemo Wafanyabiashara,wavuvi,madereva bodaboda,walimu,pamoja na vijana walijitokeza Jana Januari 25, 2025 na kueleza namna walivyofurahishwa na maamuzi ya wajumbe wa mkutano huku wakiahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha Rais Dkt.Samia anashinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu.
Viongozi wa makundi hayo walisema wajumbe walifanya maamuzi sahihi kwani Dkt.Samia amefanya mabadiliko makubwa sana katika sekta mbalimbali
“Rais Samia amefanya mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu,miundo mbinu imeboreshwa watoto wetu wanasoma vizuri hata kwa upande wa afya hali ni nzuri hivyo tunaunga mkono maazimio ya mkutano mkuu ili kwenye uchaguzi mkuu ashinde kwa kishindo azidi kutuletea maendeleo katika nchi yetu”, walisema. 
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala alisema tangu Rais Samia aingie madarakani 2021 jumla ya shilingi tirioni 5.6 ziliingizwa mkoani humo kwaajili ya kuendeleza,kuanzisha na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inagusa maisha ya watanzania
“Fedha hizo zimekwenda kwenye sekta ya maji,uendelezaji wa sekta ya elimu,uboreshaji wa sekta ya afya,pamoja na vivuko ambavyo vitasaidia kurahisha huduma ya usafiri rsala ka Mkoa wetu wa Mwanza”, alisema Masala. 
Akizungumza wakati wa kufunga Mkutano huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) MKoa wa Mwanza, Michael Lushinge ‘Smart’ alimpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu kwa kuchaguliwa kwa kishindo kwa kura zote za ndio 1924 kuwa mgombea pekee kwenye uchaguzi mkuu 2025.
Pia alimpongeza Makamu mwenyekiti Wa chama hicho Steven Wasila kwakuchaguliwa huku akisema wamepata mtu sahihi ambaye atawaongoza vizuri.