Wasanii mbalimbali na watu maarufu ni miongoni mwa watu waliohudhuria mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Lengo kuu la mkutano huu ni kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), ambayo imekuwa wazi tangu Abdulrahman Kinana alipojiuzulu tarehe 28 Julai 2024.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) ni muhimu katika kumsaidia Mwenyekiti wa chama kutekeleza majukumu yake, hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Mkutano huu unatarajiwa kutoa dira mpya ya uongozi ndani ya chama na kuimarisha mshikamano wa wanachama katika kipindi hiki cha maandalizi ya uchaguzi.
Mbunge wa jimbo Bumbuli Januari Makamba akifurahia jambo na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion na Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM Alex Msama pamoja na Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo katika mkutano mkuu wa CCM Dodoma.
Kamishana wa TRA Yusuf Mwenda kushoto akiwasili katika mkutano mkuu wa CCM jijini Dodoma