Baadhi ya Masheikh waliopata Elimu ya Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa kwa Miezi Mitatu waliohudhuria katika Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo hayo hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Baadhi ya Masheikh waliopata Elimu ya Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa kwa Miezi Mitatu waliohudhuria katika Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo hayo hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Baadhi ya Wakufunzi waliohudhuria katika Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Mmoja kati ya Masheikh waliopata Elimu ya Usimamizi wa Ndoa Sheikh Khalfan Abdulla Abdulsatar akisoma risala katika hafla ya Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Mkuu wa Divisheni ya Utafiti na Utatuzi wa Migogoro na Mjumbe wa Baraza la Maulamaa Ofisi ya Mufti Sheikh Shaban Salim Humud akizungumza kuhusiana na Migogoro ya Ndoa katika hafla ya Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Ust,Rajab Makame Ali akizungumza kuhusiana na Urajis wa Ndoa na Talaka katika hafla ya Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (watatu kulia)akitoa hotuba ya Ufungaji katika hafla ya Mahafali ya Mkupuo wa Pili wa Mafunzo ya Usimamizi wa Ndoa hafla iliofanyika Katika Msjid Jamii Zinjibar Mazizini Zanzibar.
……………
NA ALI ISSA. Maelezo 16/01/2025
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekhe Saleh Omar Kab amewata wasimamizi wa ndoa kuwafungisha ndoa wanandoa kwa kufuata sheria za dini ya kiislam.
Ameyasema hayo huko Msikiti wa Jamii Zinjibari Mazizini Mkoa wa0 Mjini Magharibi unguja katika Mahfali ya Wasimamizi wa ndoa mkupuo wa pili.
Amesema kumekuwa na migogoro mingi ya wanandoa katika jamii inayosababishwa na baadhi ya wasimamizi wa ndoa kufungisha ndoa bila ya kufuata taratibu na sheria za ndoa.
Aidha amesema wapo baadhi ya watu waliolewa ikiwa mawalii wao sio sahihi kisheria na baadhi ya wanawake kujiandikia talaka wenyewe jambo ambalo halikubaliki kisheria na hupelekea migogoro katika jamii.
Amefahamisha kuwa msimamizi wa ndoa ni lazima atizame talaka vyeti vya ndoa kwa umakini na aridhike kwani baadhi ya watu hujaribu kufoji talaka na kukosesha haki kwa mume,mke na watoto.
“tutambue kuwa amana ni kitu muhimu utapo mfungisha ndoa mtu bila kufuata taratibu za kisheria utabue kuwa umepoteza mfumo mzima wa ndoa na haki za watu ikiwemo kizazi”alisema mufti Mkuu Seleh Omar Kabi.
Nae Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar Khalid Ali Mfaume amesema Ofisi hiyo imekua ikitoa Mafunzo kwa awamu na kwa utaratibu maalum, Ili kupunguza migogoro ya ndoa katika jamii.
Aidha amesema mafunzo hayo yanahusisha sekta mbalimbali ni pamoja na wasimamizi wa ndoa kwa mashekhe,Mafunzo ya wanandoa,na Mafunzo kwa walio silimu kuingia katika uislamu.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema wanaishukuru ofisi hiyo kwa kuwapatia Mafunzo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa utaratibu wa Elimu walioipata.
Mafunzo hayo yameanza Tarehe 22/ 10/2024 hadi tarehe 8/1/2025 yalioshirikisha wasimamizi wa ndoa 175 waliofaulu 170 naTano wameshindwa kutokana na sababu mbalimbali na mada zilizojadiliwa ni Ndoa,talaka na taratibu za kufunga ndoa raiya wa kigeni.