Wekundu wa Msimbazi Simba SC imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kutoa sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Fc Bravos do Maquis wakiwa ugenini nchini Angola.
Bao la Simba SC limefungwa Leonel Ateba dakika ya 69 akisawazisha bao walilofungwa na Fc Bravos do Maquis kupitia kwa mchezaji wao Abdenego dakika ya 13.
Kufatia matokeo hayo Bravos imefunga ukarasa wa kutinga hatua ya robo fainali wakiwa na pointi 7, huku Simba SC ikiwa na pointi 10, Constatine wenye pointi 12 wakiwa wamefuzu hatua ya robo fainali kombe la shirikisho barani Afrika.