Na Mwandishi wetu, Mwanza
UMOJA wa wachimbaji vijana wa shirikisho la wachimbaji wa madini Tanzania FEMATA, wanatarajia kufanya mkutano wao wa kwanza jumapili ya Januari 12 kuanzia saa 1 jioni hadi saa 2 usiku.
Mwenyekiti wa wachimbaji vijana wa FEMATA, Magreth Baraka Ezekiel ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kikao hicho.
Magreth amesema kikao hicho kitafanyanyika kwa njia ya mtandao kupitia Google Meet kiungo kikiwa https://meet.google.com/qbo-vczd-tna
Amesema ajenda kuu itakuwa kujadili changamoto na fursa za uchimbaji kwa vijana, dira na sera ya wachimbaji kwa vijana ya mwaka 2025-20230.
“Hii ni fursa pekee mwa wachimbaji vijana kuungana, kushirikishana mawazo na kuimarisha maendeleo katika sekta ya madini,” amesema Magreth.
Mchimbaji wa madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Joseph Laizer amempongeza Magreth kwa kuandaa kikao hicho cha kwanza tangu achaguliwe.
“Mwenyekiti wa vijana ameonyesha kuwa ni jembe la kazi kwani ni hivi karibuni tuu tulimchagulia Tanga kwenye uchaguzi wa FEMATA,” amesema Laizer.