Waziri wa Maji,Nishati na Madini Mhe. Shaib Hassan Kaduara akiweka jiwe la msingi katika Jengo la Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar huko Tunguu Wilaya ya Kati, ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra ya Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe. Shaib Hassan Kaduara akizungumza wakati wa Uwekaji wa Jiwe la msingi, jengo la Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar, lililopo Tunguu Wilaya Kati, ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra ya Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ndg. Fatma Hamad Rajabu akitoa taarifa ya kitaalamu katika uwekaji wa Jiwe la Msingi, Jengo la Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar huko Tunguu Wilaya ya Kati,ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra ya Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akitoa salamu za wananchi wa Mkoa huo wakati wa uwekaji wa Jiwe la msingi, Jengo la Shirika la Magazeti ya Serikali huko Tunguu Wilaya ya Kati, ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra ya Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Magazeti ya Serikali wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Maji,Nishati na Madini Mhe.Shaib Hassan Kaduara (hayupo pichani ) katika uwekaji wa jiwe la msingi, Jengo la Shirika la Magazeti ya Serikali huko Tunguu Wilaya ya Kati, ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra ya Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Muonekano wa Jengo la Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar liliopo Tunguu Wilaya ya Kati,ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra ya Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
…………
Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe. Shaibu Hassan Kaduara amesema lengo la Serikali ni kuona Taasisi zote zinapiga hatua kimaendeleo ili kuweza kukidhi mahitaji yaliopo.
Ameyasema hayo huko Tunguu wakati wa uwekaji Jiwe la msingi Ofisi za Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra ya Maadhimisho ya Miaka ya 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema Ofisi hiyo, itasaidia kurahisisha kazi na kuipatia Serikali mapato sambamba na kuondosha changamoto mbalimbali ikiwemo kuchapisha Magarzeti katika kampuni binafsi.
Aidha Mhe. Kaduara amesema ni vyema Waandishi wa Habari kuzingatia maadili na uzalendo wa Nchi yao sambamba na kutumia kalamu zao vizuri kuielimisha jamii umuhimu wa suala la Amani na Utulivu.
Mbali na hayo Mhe. Kaduara ametoa wito kwa Waandishi ya habari kujikita zaidi kwa Wananchi wa vijijini ili kuweza kuibuwa Changamoto walizonazo.
Kwa Upande wa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmuod amesema Mkoa huo umepiga hatua kimaendeleo kwani jumla ya miradi 17, yenye thamani ya Sh.194 imeziduliwa katika maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Akitoa taarifa ya kitaalamu, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Ndg. Fatma Hamad Rajab amesema mradi huo tayari umeshafikia asilimia 50 na unatarajiwa kukamilika mwezi September 2025.
Aidha amesema Mradi huo, utaliwezesha Shirika hilo kuwa na Ofisi za kisasa, zitakazoweza kukidhi mahitaji ya uendeshaji na uwekezaji.
Ujenzi wa Ofisi za Shirika la Magazeti ya Serikali, Zanzibar, unatarajiwa kugharimu Zaidi ya Sh. Bilioni 8 ambapo litakuwa na Ghorofa 4, Kiwanda cha kuchapishia Magazeti, Nyumba mbili za Wafanyakazi, Msikiti, Majengo ya Walinzi, Jengo la Jenereta pamoja na Maegesho ya Gari.