Katika historia ya nchi yetu, mnamo Agosti 29, 2024 imetimia muongo mmoja, tangu Timu ya Serikali ya Tanzania _ikwae pipa_ kuelekea Maputo, Msumbiji kwenye kesi ya mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Malawi.
Wajumbe wa Timu hiyo ya Serikali walikuwa 7 ambapo Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, *Mhe Shamim Nyanduga* alijumuika nao. kutoka kushoto ni :
*Hamza S. Johari* (Mwanasheria). *Mhe Benard Camilius Membe* alimjumuisha *Bw. Johari* kwenye Timu hii baada ya kuvutiwa sana na _”Atikali Mujarab”_ aliyokuwa ameiandika gazetini kuhusu mgogoro huo. *Mhe Membe* ndiye alikuwa Mkuu wa msafara. *Bw. Johari* sasa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
*Mhe Patrick Luciano Tsere* aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi ;
*Mhe Deo Haule Filikunjombe* (aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ludewa)- Shahidi;
*Mhe Benard Camilius Membe* aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje;
*Mhe Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka* aliyekuwa Waziri wa Ardhi;
*Mhe Fredrick Mwita Werema* aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na
*Mhe John Damiano Komba* (aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyasa) – Shahidi