Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Saada Mkuya Salum (kulia)akikunjuwa Kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi Barabara ya Mpendae Planned Area Street Roads 6.41 km,Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu “Miaka 61 ya Mapinduzi :Amani ,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.
Na Rahma Khamis Maelezo. 1/1/2025
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dkt. Saada Mkuya Salum amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha inaboresha miundombinu ya barabara kwa wananchi Mjini na Vijijini ili kurahisisha huduma za kijamii.
Ameyasema hayo Mpendae wakati akiweka Jiwe la Msingi katika barabara ya Mpendae Planed Area street Road yenye urefu wa kilomita 6.41 ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 61 ya Mapinduzi.
Aidha amesema kuwa lengo la Serikali kuhakikisha barabara zote za Zanzibar zinajengwa kwa kiwango cha lami na kusema kuwa watahakikisha barabara zote zinakamilika kwa kiwango hicho ikiwemo na zile zinaendelea kujengwa ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Amesema ni ujenzi wa barabara hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya chama Cha Mapinduzi katika kutekeleza ahadi zake alizozitoa kwa wananchi wake.
“Tunajua kwamba unatekelezea Ilani ya chama na una wasimamimizi wako ambao wanasimamia Ilani hiyo” alisema Waziri.
Hata hivyo amewataka madereva na watumiaji wengine kuitumia barabara hiyo kwa usalama zaidi ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.
Akitoa taarifa ya kitaalamu kuhusu barabara hiyo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Hawaa Ibrahim Mbaye amesema kuwa eneo la Mpendae limebahatika mradi wa barabara za Mjini zenye urefu wa 157 ambazo zinajengwa na Mkandarasi kutoka China ( CCECC).
Aidha amefahamisha kuwa ujenzi hiyo umezingatia madaraja, miundombinu ya kupitisha Maji ya mvua, njia za watembeza kwa miguu, alama za usalama barabarani, taa, pamoja na kuzingatia mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum.
Nao wananchi wa eneo hilo wamesema kuwa wamefurahishwa kuona barabara hiyo kwani itaweka mazingira mazuri na yenye kuvutia, NUjenzi wa barabara hiyo umegharimu Dola za Kimarekani milioni 116 laki moja thalini moja mia nane arubaini na mbili .96.