Na Ali Issa, Maelezo
Naibu Spika wa Baraza la wawakilishi Zanzibar Mhe,Mgeni Hassan Juma Amesema kumalizika kwa Kituo cha Afya Tunguu kitapunguza tatizo la kufuata huduma za afya masafa marefu kwa Wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.
Ameyasema hayo wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi wa kituo cha Afya Tunguu wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja kufuatia shamrashamra za kutimiza miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema kituo hicho ni kituo cha kisasa na kitakuwa na ubora wa hali ya juu kutokana na kituo hicho mipango yake ipo katika daraja bora la vituo vitakavyo kuwa na huduma muhimu ikiwemo kufanya vipimo vya uchunguzi XRAY,Utrasaund kufanya upasuaji, kulaza wagonjwa na kutoa huduma nyenyinge muhimu kwa mama na mtoto.
“Mimi ni wambie tu kituo hiki kitatoa huduma za hospitali wilaya ambazo zitapatikana hapa ni jambo jema kwani litapunguza kupelekea msongamano katika vituo vyengine” alisema Mgeni Hssan.
Aidha Mhe,Mgeni aliwataka wananchi wa maeneo hayo pamoja na yajirani kukitumia kituo hicho mara baada ya kumaliza na kukituza ili kiweze kudumu kwa Muda mrefu na kiwe na manufaa kwa vizazi vya sasa na vya baadae.
Nae Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Amuor Seleiman Mohamed akisoma taarifya ya kitalam alisema jengo hilo la ghorofa moja liliaza ujenzi wake Julai 15 /2023 mara tu baada ya kufanya usafi na kuvunja kituo kidogo kilichokuwepo awali na unatarajiwa kumaliza mei 25/2025 na
Aidha alisema kwa sasa zanzibar jumla ya vituo 142 ambao dispensary ni 90 na vituo kama hivyo 52 badala ya vile vya awali walivyo naavyo 169 ambapo serikali pia itaimarisha kwa kujenga upya vituo vya afya katika wilaya zote unguja na pemba kwa lengo la kuwaekea karibu wananchi huduma za afya.
Mapema mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayuob Muhamed Mahmuod amesema katika miradi nane kati ya miradi 17 waliopanga kufungua na kuweka mawe ya msingi katika mkoa wake lakini katika sekta ya Afya mradi huo ni mradi wa tatu na huo ni mradi wa mwazo kuekewa jiwe la msingim kwa sekta ya afya.
Mkuu wa mkoa huo alishukuru jitihada za maraisi Husseni Mwinyi na Rais Samiya Suluhu Hassan kwa jitihada zao wanzo zifaya kwa mkoa wake kwa kuipatia Zanzibar gawiyo lake pesa zinazo tokana na taasisi za muungano na gawio la kovid 19 ambazo zimeisaidia mkoa wa kusini unguja.
Jumla ya Bilioni 3 na milioni 600 fedha za serikali ya SMZ zinatarajiwa kutumikakujenga ujenzi huo na kitahudumia watu zaidi ya laki 177647 ambao wakazi wa jumbi,binguni na tunguu na maeneo jirani na ujenzi wake umefikia asilimia 52.