Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Hope Mahokola (kushoto) ambaye ni Afisa Masoko wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambaye alitoa maelezo kuhusu majiko yanayotumia umeme kidogo, wakati alipotembelea banda la maonesho la STAMICO katika Tamasha la Azimio la Kizimkazi lililofanyika Kilimahewa Majumbakumi, Ruangwa, Desemba 31, 2024. Kulia kake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi , Zainab Telack, wa pili kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TBC, Nestory Madirisha na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Radio TBC, Anna Kwambaza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)