Na Prisca Libaga, Kilimanjaro
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 23.12.2024 imetoa elimu kinga kwa umma juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya katika mbio za Rombo Marathon na Ndafu Festival zilizofanyika eneo la Rongai wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro.
Mgeni rasmi katika mbio hizo alikuwa ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye mwenyeji wake alikuwa ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb).
Washiriki wa mbio hizo walihamasishwa kushirikiana na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kupitia namba ya simu ya bure ya 119.




