Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Disemba 24,2024 amefanya ziara ya kushitukiza katika kiwanda cha Hope Recycling kilichoko Kigogo Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila akiwa katika kiwanda hicho alitembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji ndani ya kiwanda ikiwemo sehemu ya uchakataji taka za plastic, uundaji wa TV, bati, motor na vifaa vya majumbani.
Aidha Mhe Mkuu wa Mkoa alionyesha kutoridhishwa na namna kiwanda hicho kinavyoendesha uzalishaji wa bidhaa hususani ubora wa bidhaa zinazozalishwa, mifumo ya maji taka pamoja na matumizi ya mashine ya EFD katika ulipaji wa kodi.
RC Chalamila amesema Serikali inatambua na kuthamini uwekezaji wa wazawa na hata wageni lakini katika uwekezaji huo ni lazima kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali ikiwemo kulipa kodi asiwepo mwekezaji au mtu yoyote anayekwepa kodi.
Mwisho RC Chalamila amewataka wawekezaji wote katika Mkoa huo kufuata sheria na taratibu zizowekwa ili waweze kufanya biashara kwa uhuru lakini pia kwa masilahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla kwa kuwa kupitia uwekezaji fursa mbalimbali hupatikana kama vile ajira.