Mstahiki Meya Manispaa ya Sumbawanga Justine Malisawa akizungumza katika mkutano huo.
Wajasiliamali waliopatiwa mafunzo na kunufaika na mkopo huo.
Mfano wa Hundi ya fedha iliyotolewa
Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Ayesh Khalifan Hilary wakati akizungumza na wajasiliamali katika ukumbi wa manispaa ya Sumbawanga.
Picha Neema Mtuka.
………………….
Na Neema Mtuka Sumbawanga
Wajasiliamali manispaa ya Sumbawanga Watakiwa kuwa na nidhamu ya fedha na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kunufaika na mikopo.
Hayo yamesemwa Leo Desemba 24, 2024 na Katibu Tawala wilayani ya Sumbawanga Gabriel Masinga wakati wa kutoa mafunzo ya namna ya kutumia fedha watakazo kopa .
Amesema wajasiliamali Wamepewa kanuni za kwenda kufanya uzalishaji wenye tija kwa bidii ili wairudishe na wengine kukopa tena.
Akifungua mafunzo hayo leo Disemba 24/2024, Katibu Tawala wa Wilaya ya Sumbawanga Gabriel Masinga amewahimiza wanufaika hao kwenda kufanya uzalishaji wa fedha na kuongeza kipato kwa kasi ikiwa ni pamoja na ubunifu katika biashara ili kupata matokeo chanya kwa maendeleo endelevu ya uchumi na biashara zao.
Pamoja na hayo Masinga amewaasa wanufaika hao kuwa na nidhamu ya fedha na kuachana na matumizi holela ya fedha ili kuinua uchumi binafsi hatua itakayoleta maendeleo makubwaa ya Jamii.
Kikundi cha Mshikamano Kanondo na Annointed Group ni miongoni mwa vikundi 14 waliopatiwa mafunzo na ni wanufaika wa mkopo huo ndani ya Manispaa ya Sumbawanga, wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha za mkopo kwa vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu na kuahidi kuzingatia elimu ya fedha waliyopatiwa.
“ili tutimize malengo tuliyojiwekea kwa maendeleo yenye tija tutahakikisha tunazitimia pesa hizo vizuri ili zitusaidie.
Katika hatua nyingine afisa maendeleo ya Jamii manispaa ya Sumbawanga Frank Mateni amesema jumla ya vikundi 14 vimepewa mkopo wenye thamani ya Tshs 223,000,000ili kwenda kujiinua kiuchumi.
Mateni amesema vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu waliyoomba mikopo ndani ya muda wa dirisha la mikopo na vinavyotarajiwa kupatiwa mikopo hiyo ya asilimia kumi kwa robo ya pili ya Oktoba Hadi Desemba ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Vikundi 9 vya wanawake vikundi 4 vya vijana na kikundi kimoja Cha watu wenye ulemavu wamenufaika na mkopo huo.
Tangu kufutwa kwa huduma ya mikopo kutolewa kwa Halmashauri kote Nchini mkoa wa Rukwa umeanza na dirisha la mikopo kwa robo ya pili ili wananchi wanufaike.
Akizungumza katika hafla ya utoaji wa mikopo mgeni rasmi mbunge wa Jimbo la Sumbawanga AESH Khalifan Hilary amemtaka Mkurugenzi ahakikishe wanawake wa vijijini wanapewe kipaumbele ili nao wanufaike .
Amesema kuwa mikopo hiyo imetolewa kwa mujibu wa Sheria ya mikopo iliyopo hivi sasa.
“Nina Imani nao kuwa hata wao wanastahili kupata mikopo hiyo na wanaweza kurejesha you kwani wanawake wanaweza”.amesema Aesh.
Jamila Nandi ambaye ni mnufaika wa mkopo huo kutoka kikundi Cha Moto Moto amesema ataendeleza biashara yake ya vitenge ili kujiongezea kipato na kurudisha kwa uaminifu.
“Tumepewa mafunzo ya kutunza fedha na namna ya uzalishaji tutazingatia yote tuliyofindishwa ili tueendelee kuaminiwa”.
Samson Ngeleza ni kijana anayeishi na ulemavu kutoka kata ya Mtimbwa amesema anaishukuru Serikali kwa kupata mkopo huo na atauendeleza ili uzae matunda.
Ameitaka Serikali kuendelea kuwashika mkono kwani hata wao wanaweza kufanya kazi na kuacha tabia ya kuomba omba ili hali wakipewa mikopo wanauwezo wa kufanya kazi.
Mada zilizofundishwa ni pamoja na taratibu za utoaji mikopo kulingana na kanuni na mwongozo wa mikopo ya asilimia kumi, fursa za mikopo na mitaji, utunzaji wa kumbukumbu, biashara ujasiliamali na uwekezaji, elimu ya sheria na ujazaji wa mikataba, usajili wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wadogo.