Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba wakati wa Mazishi ya Bi. Margret Ntibayizi ambaye ni Mama wa Mkuu wa Mkoa huyo
yaliyofanyika Mwandiga mkoani Kigoma leo tarehe 24 Desemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki Ibada ya Mazishi ya Bi. Margret Ntibayizi ambaye ni Mama wa Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe. Peter Serukamba iliyofanyika Mwandiga mkoani Kigoma leo tarehe 24 Desemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa salamu za rambirambi kwa waombolezaji mbalimbali mara baada ya Ibada ya kumuaga marehemu Bi. Margret Ntibayizi ambaye ni Mama
wa Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe. Peter Serukamba iliyofanyika Mwandiga mkoani Kigoma leo tarehe 24 Desemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka mchanga katika kaburi la Bi. Margret Ntibayizi ambaye ni Mama wa Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe. Peter Serukamba wakati wa Mazishi
yaliyofanyika Mwandiga mkoani Kigoma leo tarehe 24 Desemba 2024
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiweka shada la maua katika kaburi Bi. Margret Ntibayizi ambaye ni Mama wa Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe. Peter Serukamba wakati wa Mazishi
yaliyofanyika Mwandiga mkoani Kigoma leo tarehe 24 Desemba 2024
…………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Mpango leo tarehe 24 Desemba 2024 ameshiriki Mazishi ya Bi. Magreth Ntibayizi ambaye ni Mama wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba yaliyofanyika Mwandiga
mkoani Kigoma.
Akitoa salamu za rambirambi katika msiba huo, Makamu wa Rais amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anawaombea faraja na kuungana na familia, ndugu , jamaa na marafiki katika kipindi kigumu
kufuatia msiba huo.
Makamu wa Rais ametoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba , Familia pamoja na wote walioguswa na msiba wa Bi. Magreth Ntibayizi na kuwasihi kuendelea kumuombea apumzike kwa amani.
Amesema ni muhimu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha ya Bi. Ntibayizi aliyoishi hapa duniani ikiwemo kwa malezi aliyotoa kwa watoto wake na mchango wake katika kusaidia ujenzi wa nyumba ya Ibada.
Makamu wa Rais amewashukuru wote waliojitokeza katika kuifariji familia wakati huu wa msiba pamoja na wale walioshiriki katika kumhudumia Bi.Magreth enzi za uhai wake wakiwemo Madaktari na Viongozi wa Dini.
Ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kushirikiana wakati wa changamoto mbalimbali pamoja na kushiriki katika mafunzo ya kidini ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili ambao umechochea vitendo vya ukatili dhidi ya watoto,
wanawake, uhalifu na mauaji.
Halikadhalika, Makamu wa Rais amewaasa Watanzania hususani vijana kuwakumbuka na kuwahudumia wazazi wao katika nyakati zote.