Na Ashrack Miraji Fullshangwe Media
Mkuu wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amesema hadi kufikia asubuhi ya Desemba 23 mwaka huu 2024, mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo zimesababisha madhara makubwa ikiwemo vifo vya watu Sita.
Mvua hizo pia zimeharibu mazao, takribani Nyumba 25 kubomoka ka bisa, miundombinu ikiwemo barabara hasa zinazoelekea kata za milimani na kufanya baadhi ya maeneo kutofikika kiurahisi.
“Nitoe pole kwa ndugu na jamaa walioathiriwa na majanga haya yaliyosababishwa na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hapa wilaya ya Same mungu azilaze roho za wapendwa wetu mahara pema peponi ameen”. Alisem mkuu huyo wa Wilaya.
Kwa mujibu wa taarifa ya kamati ya maafa ya wilaya hiyo maeneo yaliyo athiriwa zaidi ni pamoja na kata za Msindo,Vuje, Bombo ,Mtii na Maore ambako bado serikali inaendelea kufanya tathimini kupitia kamati ya maafa wilaya kujua ukubwa wa athari za mafuriko hayo kwa ajili ya kupeleka taarifa hiyo ofisi ya mkoa kwa ajili ya kufikisha taarifa hizo ofisi ya waziri mkuu kwa hatua zaidi.
Aidha amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuendelea kuwa na tahadhari ikiwemo kuhama kwa muda katika maeneo hatarishi kuepusha madhara zaidi akiwataka pia wakazi waliokwenye maeneo yaliyokubwa na maafa kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati Serikali ikiendelea na tathimini ya athari ya mafuriko hayo lakini pia mipango inaendelea kurudishia miundombinu yote iliyoharibiwa na Mvua.