Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa amekabidhi vifaa vya michezo kwa Timu ya michezo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) ambapo vimepokekewa na viongozi wa timu hiyo wakiongozwa na Bw. Shabani Maganga na Micdad Magola.
Shughuli ya makabidhiano imefanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam Desemba 21, 2024.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na seti 5 za jezi, mpira wa miguu, soksi, viatu vya kuchezea mpira wa miguu, Trakisuti pamoja na Raba
Balozi Mussa ametoa pongezi kwa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajabu na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Hamis Mussa kwa juhudi zao kubwa za kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinapatikana.
“Nawapongeza na asante sana kwa mabalozi wetu hawa, Mhe. Balozi Fatma Rajabu na Balozi Mussa kwa jitihada zao za kufanikisha upatikanaji wa vifaa vya michezo kwa ajili ya Timu ya Michezo ya Wizara,” Alisema Balozi Shaibu.
Balozi Mussa ameeleza kuwa upatikanaji wa vifaa hivvyo vitaisaidia timu hiyo kushiriki na kuendelea kufanya vizuri kwenye michezo mbalimbali iliyopo mbele yao.
Pamoja na mambo mengine Balozi Shaibu alitoa rai kwa watumishi wa Wizara kuendelea kushiriki kwenye michezi, kwa kuwa kupitia michezo afya ya mwili inaimarika na kukuza upendo na udugu baina ya watumishi.
Kwa Upande wa Kocha wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje – Sports) Bw. Shaban Maganga ameushukuru Uongozi wa Wizara ukiongozwa na Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuwaunga mkono kwenye kuhakikisha Nje – Sport inashiriki na kufanya vyema kwenye Michezo.
“Kwakweli tuna furaha kubwa kuupokea mzigo huu wa vifaa vya michezo kwani vutatuongezea Motisha na Morali wa kuendelea kufanya vizuri na kuleta Ushindi, Tunamshukuru Balozi Fatma Rajabu pamoja na Balozi Hamis Mussa kwakutuletea Vifaa hivi vizuri vya michezo” Alisema Bw. Maganga
Ikumbukwe Nje – Sports imekuwa ikifanya vizuri kwenye michezo inayoshiriki, Mara ya Mwisho Nje – Sports iliibuka Mshindi wa Tatu kwenye Michezo ya Shimiwi iliyokuwa inatimua vumbi Mkoani Morogoro, Sasa imeelekeza nguvu kwenye michuano ya Mapinduzi itakayofanyika Visiwa vya Marashi ya Karafuu Zanzibar.