Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na wananchi mbali mbali wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi Viwanja vya Maisara,Wilaya ya Mjini, ikiwa ni miongoni mwa Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akitoa maelezo kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi viwanja vya Maisara,Wilaya ya Mjini ikiwa ni miongoni mwa Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Wizara wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ndg. Fatma Hamad Rajab akitoa taarifa za kitaalamu kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi(hayupo pichani) wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi Viwanja vya Maisara,Wilaya ya Mjini ikiwa ni miongoni mwa Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ndg. Fatma Hamad Rajab akicheza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi viwanja vya Maisara,Wilaya ya Mjini ikiwa ni miongoni mwa Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya Wafanyakazi na Wananchi sambamba na Masheha wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi Viwanja vya Maisara,Wilaya ya Mjini ikiwa ni miongoni mwa Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
……..
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ataendelea kujenga viwanja vya kisasa kupitia mradi mkubwa kwa Wilaya na Mikoa ya Unguja na Pemba lengo ni kuengeza vipaji kwa vijana .
Amesema hayo huko Maisara Wilaya ya Mjini, Unguja wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi Viwanja vya Michezo Maisara ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra ya Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema kutakuwa na Academ maalum kwa kila mkoa ili vijana waweze kupatiwa mafunzo ya michezo mbali mbali ili kuibua vipaji vya michezo nchini .
Aidha amesema miongoni mwa ujenzi wa viwanja hivyo kutakuwa na ukarabati mkubwa wa viwanja viwili vya kitaifa ikiwemo kiwanja cha Mau-Zedong na Gombani, Pemba ili kurejesha hadhi yake .
Ameeleza kwamba Kiwanja kipya kinatarajiwa kujengwa chenye kiwango cha kimataifa, kwa ajili ya Bearch Soka ambacho anafikiria kujenga Olympic site Swimming pool kwa ajili ya vijana wa mashindano ya michezo ya kuogelea, sambamba na Mradi mkubwa wa ujenzi wa Kiwanja cha Afcon ambacho ni cha aina yake .
Amesema Zanzibar inajiandaa na mashindano makubwa ya mpira wa miguu kwa wachezaji wa ligi za ndani CHAN ifikapo Febuari 2025 .
Ameeleza kuwa Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar ni ‘’Amani Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo ya Taifa’’ hivyo amewataka wananchi kuhakikisha wanadumisha amani iliyopo wasikubali kufitinishwa .
Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema kuwa Wizara ya habari itaendelea kutekeleza maelekezo yaliyopangiwa ikiwemo kumalizika kwa miradi yote ifikapo April 2025.
‘’Tuko tayari na tutaendelea kutekeleza mema na mazuri unayotuongoza, Tutahakikisha yale yote tunayoyafanya yamo kwenye maelekezo yako ‘’amesema Mhe. Tabia .
Amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa juhudi zake za kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020 -2025 kwa asilimia 100 kwa kueneza viwanja vya michezo nchi nzima .
Aidha amesema katika Ilani hiyo imeeleza kuimarisha miundombinu ya michezo kwa kuzisaidia na kuzisimamia Timu za Taifa, Zanzibar Herous na Karume Boys iliyoleta ubingwa ndani ya uongozi wa awamu ya nane ikiwa ni ishara tosha ya utelezaji wa ilani kwa vitendo.
kwa Upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Ndg. Fatma Hamad Rajab akitoa taarifa za kitaalamu amesema viwanja hivyo ni miongoni mwa mradi mkubwa wa viwanja 17 ambavyo vinaendelea kujengwa kwa Unguja na Pemba.
Amefahamisha kuwa ujenzi wa kiwanja hicho umefikia asilimia 60 kwa sasa ambao umeanza Septemba 2024 na kutarajia kumalizika kwake mnamo mwezi March 2025 .
Alimshukuru Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na michezo kwa kusimamia vyema wizara hiyo jambo ambalo limeleta mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.