Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 2 – 0 dhidi ya Ken Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliochezwa leo Disemba 18, 2024 katika Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na Mshambuliaji Leonel Ateba dakika ya 35 kwa changamoto ya mkwaju wa penalti iliyosababishwa na Awesu Awesu na dakika ya 44 kwa pigo la kichwa akimalizia kona iliyopigwa na Nouma.
Kufatia matokeo hayo Simba SC nimefikisha pointi 31 ndani ya ligi, huku Ken Gold ikisalia na pointi zake sita baada ya kucheza mechi 15.