***************************
NA FARIDA SAIDY MOROGORO
Zoezi la daftari la kudumu la wapiga kura linatarajiwa kufanyika kwa siku saba kuanzia januari 23 hadi 29, 2020 katika mikoa ya Morogoro na Tanga.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Mhe Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage Katika mkutano wa tume na wadau wa uchaguzi mkoa wa Morogoro uliofanyika januari 15, 2020 katika ukumbi wa mkuu wa mkoa.
Jaji Kaijage amesema mpaka sasa tume imeshakamilisha maandalizi kwaajili zoezi hilo kwa mikoa ya morogoro na Tanga na kwamba uboreshaji wa daftari la wapiga kura tayari ulikwisha anza kwa mikoa 25 ya Tanzania bara na zanzibar tangu kuanzishwa kwake july 18,2019
Mkoani kilimanjaro.
Amefafanua kuwa miongoni mwa maboresho yanatarajiwa kufanyika ni pamoja na kufanyika marekebisho kwa mwananchi ambaye alijiandikisha katika kituo kingine na amehama eneo hilo kwamba taarifa zake zitaweza kurekebishwa kulingana na eneo alipo.
Mwenyekiti mh. jaji kaijage ameeleza kuwa uboreshaji wa safari hii hauhusishi wapiga kura wote walioandikishwa 2015, bali uboreshaji huu utawahusu wapiga kura wapya ambao wametimiza au watatimiza umri wa miaka 18 mwaka huu 2020 siku ya uchaguzi mkuu.
Katika upande wa elimu ya mpiga kura ameeleza kuwa inaendelea kutolewa kupitia vyombo ya habari, gari la matangazo la tume ya uchaguzi ambalo limekua likipita maeneo baadhi ya maeneo, kwenye mikusanyiko ya watu kama vile sokoni na matamasha pia mitandao ya
kijamii.