Meneja wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Kanda ya Kati Joseph Sayi (kushoto) akimkabdhi cheti mwanafunzi Winnie Futa wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa kike katika masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yaliyofadhiliwa na Vodacom.
Meneja wa Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania Kanda ya Kati ,Joseph Sayi (kulia) akizungumza na wanafunzi wasichana kutoka Kanda hiyo wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Udom Jijini Dodoma jana kwa ufadhili wa Vodacom.
Baadhi ya wanafunzi wa kike kutoka shule za sekondari Kanda ya kati wakijifunza jinsi ya kutumia kopyuta kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA ) yaliyofanyika Chuo kikuu cha Udom Jijini Dodoma jana kwa ufadhili wa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania.
Meneja wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Kanda ya Kati Joseph Sayi (kushoto) akimkabidhi begi mwanafunzi Emmeline Kitali wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea wanafunzi wa kike uwezo wanafunzi wa kike katika masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yaliyofanyika Chuo kikuu cha Udom Jijini Dodoma jana kwa ufadhiliwa na Vodacom.