Wakili wa serikali mkuuWizara ya Katiba na Sheria Richard Jacopiyo amewataka viongozi wa kuchaguliwa ,wakuteuliwa na watendaji wa kata kuacha kupandisha mabega katika kuongoza Wananchi badala yake watekeleze Utawala wa kisheria kwenye Maeneo yao ya kuwahudumia.
Jacopiyo ametoa kauli hiyo Wakati akizungumza na viongozi wa kamati za Usalama,wakuu wa idara mbalimbali Halmashauri ya Wilaya ya Butiama Mkoani mara.
“Tukitambua swala la kuwahudumia Wananchi bila kupandisha mabega viongozi wote wakuteuliwa wakuchaguliwa lazima tutaenda kwa namna ambavyo inatakiwa maana Sisi niwajibu wetu kuwahudumia.
Pia Alisema wapo baadhi ya viongozi walioko kwenye mamlaka wamekuwa miungu watu katika kutoa huduma Kwa wananchi nahili linapeleka kuichukia Serikali yao ambapo amewataka viongozi hao kwenda kubebe dhamana zao katika kutoa huduma Bora kwa Wananchi.
“Kama viongozi wa serikali naamini mnafaham Falsafa ya Rais DKT Samia Suluhu Hassan ya 4R Ile Falsafa kuangalia kwa undani inaboresha Utawala Bora na demokrasia na Utawala bora kwahiyo ukiangalia pale kila mtanzania ajivunie kuwa mtanzania nanikweli nahilo ndio lengo la Mheshimiwa DKT Samia Suluhu Hassan tembeeni kwenye Njia hiyo”Alisema Richard Jacopiyo wakili Mkuu wa Serikali Wizara ya Katiba na sheria.