Na Prisca Libaga Arusha
Washiriki wa Mkutano huo waridhishwa na kupongeza jitihada za Serikali katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini.
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 13.12.2024 imewaongoza kutembelea Kituo cha Matibabu kwa Kutumia Dawa ya Methadone (MAT Clinic) kilichopo katika hospitali ya Rufaa ya mount MERU iliyopo jijini Arusha washiriki wa Mkutano wa Umoja wa Afrika waliokuwepo jijini Arusha wakijadili masuala mbalimbali ikiwemo namna bora zaidi ya kupunguza uhitaji wa dawa za kulevya balani Afrika.
Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kujifunza jinsi nchi ya Tanzania inavyoratibu huduma za matibabu na utengamao kwa waraibu wa dawa za kulevya chini ya usimamizi wa DCEA.
Washiriki wa Mkutano huo uliodumu kwa siku nne walielezwa mafanikio ya Serikali katika kuboresha na kupanua wigo wa kutoa huduma ambapo hadi kufika Disemba 2024 kuna vituo cha MAT Clinic 17 na Nyumba za Upataji Nafuu 56.