Wekundu wa Msimbazi Simba Sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia katika mchezo wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliochezwa leo Disemba 15, 2024 katika uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.
Simba Sc ilipata goli lake dakika ya saba kupitia kwa Kibu Denis aliyesawazisha baada ya Haji Hassen kutangulia kufunga kasha kuongezwa la pili kwa mfungaji yule yule katika dakika za nyongeza.
Kufatia ushindi huo Simba Sc imefikisha pointi sita katika michezo mitatu ya hatua ya makundi ambapo inatarajiwa kuwa ugenini kurudiana na CS Sfaxien Januari 5, 2025.