Na. Edmund Salaho, Arusha
Awamu ya pili ya Semina ya waongoza watalii inaendelea katika ukumbi wa Olasiti jijini, Arusha. Semina hiyo inalengo la kujiandaa na msimu mwingine wa Utalii unaoanza Decemba 2024 hadi Februari 2025.
Semina hiyo imeandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro inaongozwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utalii, Nkoba Mabula.
Kupitia semina hii waongoza watalii wanaendelea kujenga uelewa wa pamoja juu ya taratibu mbalimbali zilizopo katika hifadhi ili kuwa na utalii endelevu lakini pia kuhakikisha watalii wanaotembelea hifadhi hizo wanapatiwa huduma bora.
Awamu ya kwanza ya semina hiyo ilifanyika tarehe 12, Decemba ambapo waongoza watalii zaidi ya 750 walihudhuria huku mada mbalimbali kama Huduma Bora kwa wateja, Uzalendo, Ukarimu, Protokali kwa wageni, Changamoto na fursa za Utalii, Sheria na taratibu mbalimbali zilizowekwa na Serikali katika maeneo ya utalii zilifundishwa.