Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Christopher Ngubiagai akizungumza kwenye hafla ya usiku wa waandishi wa habari na wadau wa habari kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda
……………..
Na Hellen Mtereko Mwanza
Waandishi wa habari na wadau wamekutana pamoja katika hafla ya usiku wa waadishi wa habari na wadau wa habari Mkoa wa Mwanza (Media Stakeholders Night Gala 2024) kwa lengo la kufurahi pamoja na kubadilishana uzoefu wa shughuli zao.
Hafla hiyo iliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC) imefanyika usiku Ijumaa Desemba 13, 2024 Katika ukumbi wa Mwanza Hotel Jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Christopher Ngubiagai kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda.
Ngubiagai amesema vyombo vya habari ni muhimili muhimu hivyo waandishi wa habari wanawajibu wa kutumia kalamu zao kwa usahihi hatua itakayosaidia kuepukana na migogoro.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa MPC Bw. Edwini Soko alisema hafla hiyo ni utaratibu wa kila mwaka kuwa na usiku wa pamoja na wadau wa habari ambao wanashirikiana katika kazi ya kufikisha maudhui mbalimbali kwa jamii.
Wadau wa habari walioshiriki katika hafla ya usiku wa waandishi wa habari na wadau wa habari ni Tashico,Nhif,Tcra,Nssf,Tira,Jeshi la Polisi,Bodi ya Pamba pamoja na Tcb