Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Elizabeth Gumbo akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji na Wasimamizi wa Vituo vya kutolea Huduma za Afya baada ya kupata mafunzo kuhusu Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii yaliyofanyika Shule ya Sekondari Maposeni Kata ya Peramiho, Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Elizabeth Gumbo akizungumza na Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji na Wasimamizi vya Vituo vya kutolea Huduma za Afya baada ya kupata mafunzo kuhusu Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii yaliyofanyika Shule ya Sekondari Maposeni Kata ya Peramiho, Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ukumbi wa Jenista Joakim Mhagama Hall .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Elizabeth Gumbo akiwa katika picha ya pamoja na uwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa baada ya kufika Ofisi kwake katika zoezi la mafunzo ya Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji na Wasimamizi wa Vituo vya kutolea Huduma za Afya katika Halmashauri hiyo Kuhusu Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.
………..
Na. Elimu ya Afya kwa Umma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Elizabeth Gumbo ametoa onyo kwa Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kuacha Upendeleo katika mchakato wa kuwapata Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.
Gumbo ametoa onyo hilo katika Ufunguzi wa Mafunzo elekezi ya Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kwa Maafisa Watendaji wa Kata 16,Maafisa Watendaji wa Vijiji 56 na Wasimamizi wa Vituo vya Huduma za Afya 45 wa Halmashauri hiyo yaliyofanyika Shule ya Sekondari Maposeni Kata ya Peramiho, Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jenista Joakim Mhagama Hall .
“Mhudumu wa Afya Ngazi ya Jamii anayeomba yeye maombi ndiye anayefanya kwa ufanisi, Watendaji wa Kata na vjiji acheni upendeleo kwa kuleta watu wenu”
Aidha, Mkurugenzi huyo wa Halmashauri amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wana mchango Mkubwa katika Jamii.
“Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ni muhimu kwa Sababu wao ndio kiungo cha Serikali pamoja na jamii na wanarahisisha kufikisha Elimu ya Afya haraka ,mfano Elimu ya Lishe na chanjo na wanaongea lugha moja na wananchi kwani wanatoka kwenye maeneo ya jamii husika”amesema.
Kwa upande wao baadhi ya Maafisa Watendaji akiwemo Rajab Tamimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Parangu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Maafisa Watendaji wa Kata katika Halmashauri ya Songea pamoja Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Peramiho B Rehema Nombo wamesema kupitia mafunzo hayo itawarahisishia usimamizi uchaguzi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii huku wakiipongeza Serikali kwa kuja na Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika Mkoa wa Ruvuma. Jumla ya Watumishi 117 wamepata Mafunzo hayo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.