EQUITY Bank Tanzania imesema itahakikisha fedha inazowapatia Wajasiriamali wanawake kuwa wanafanyia mambo ya maendele yatakayo kuza biashara zao.
Hayo alisemwa na Meneja wa Wanawake Kitengo cha Vijana Equity Bank Tanzania, Jacqueline Temu wakati mkutano wa kibiashara wa wanawake wajasililriamali ulioandaliwa hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Alisema wamefikia hatua hiyo kwa sababu watu wengi wao wakipata pesa kwa vile hawana elimu ya pesa hivyo wanajikuta wanaingia kwenye madeni baadala ya fedha hizo kuwasaidia zinawaletea matati.
“Mwaka huu mwezi wa tano tulianzisha dirisha la wanawake na tunaelewa mahitaji ya wanawake ni zaidi ya pesa kunawanawake wanapesa lakini wana changamoto kwa hiyo sisi Equity Bank Tanzania
Tupo kwa ajili ya kuhakikisha wale wanawake pesa tunazowapatia wanazifanyia mambo ya maendeleo,”alisema Temu.
Alisema kutokana na mazingira hayo wao wanawapatia elimu ya fedha na uwekezaji namna gani ya kuweka malengo, kuweka bajeti na mnagani wanaweza kujitenganisha na biashara zao.
“Lakini pia ni namnagani wanaweza kusogea kupitia biashara zao, hayo yote yanafanyika na equity Bank lakini ikiwa ni eneo la kwasisitiza wanawake waendelee kukuwa kiuchumi sawa sawa na mipango yetu katika dirisha letu la mwanamke Plus,”alisema Temu.
Meneja Mafunzo wa Equity Bank Tanzania, Martin Rajab alisema “leo hii tupo kwenye kuanzisha program maalum kwa ajili ya mafunzo ya elimu ya fedha na elimu ya biashara ambayo ni mafunzo ya vitendo.
“Ambapo tunaianza program hii ambapo ni program yam waka mzima… kwa utafiti uliofanyika wafanyabiashara wengi wanakosa elimu ya fedha na elimu sahihi ya biashara sasa tumeshazoea taasisi nyingi za fedha, mashirika mengi yamekuwa tukiendesha semina kwa ajili ya wafanyabiashara.
Mkurugezi Mtendaji Cort Limited, Cotrida Kagaruki, alisema kazi yao kubwa wanajishuhurisha na biashara ya ‘buchering,, nafaka na matunda.
“Tumekuwepo kwenye semina hii ya ADC wakishirikiana na Equity Bank, tumepatiwa mafunzo mazuri ambayo yatatusaidia kuendelea kusimamia na kuratibu biashara zetu.
“Sisi kama wafanyabiashara tukikaa pekeetu tunaweza tukafikiri tunaelewa kumbe kuna maeneo tunapata vi kwazo mbalimbali lakini tunapokaa na wataalamu ambao wanafani mbalimbali za kutusaidia.
“Kwa mfano kama leo tumekuwa na somo zuri sana kuhusu utawala wa fedha, kusimamia mradi kuwa na mpango mkakati na sio kujiendea tu na matumizi mazuri ya hiyo pesa, pesa ambayo tunaitumia tunaitumiaje.
“Lakini pia sisi kama wanawake tumekuwa tukihudhuria semina mbalimbali sasa tofauti hii semina hii semina imekuja kivingine, kwa sasa watakuwa wanafanya kwa kuja kwenye biashara zetu, kuangalia wapi tunafanya vizuri wapi tunakosea,”alisema Kagaruki.
Mkurugezi wa Kampuni ya ADC Tanzania LTD, Ester Kitoka, alisema kazi yao kubwa ni kutoa ushauri wa biashara mbalimbali ndogo na za kati wakishirikiana na wadau mbalimbali nchi na wa Kimataifa.
“Leo tupo hapa kwaajili ya program yetu ya ambayo tumeianzisha tukishirikiana na Wadau wawili wa kubwa tunashirikiana na ‘African guarantee fund’ anvayo chini ya Afriacan Develop Bank.
“Program hii ni kwa ajili ya kuwasaidia wanawake, wajasiriamali katika kuwajengea uwezo ili waweze kupata mikopo katika benki ya Equity.