Naibu Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe amepokea Magari sita yaliyotolewa na Amref Health Africa kwaajili ya usimamizi shirikishi wa shughuli za Afya katika Mikoa ya Mara na simiyu.
Magari hayo yamekabidhiwa kwa Mikoa hiyo ikiwa ni awamu ya pili ambapo awali magari mawili yalikabidhiwa Kwa Mkoa wa Simiyu na sasa Amref imetoa Magari Nne ambapo matatu yataenda Mkoa wa Mara na moja Simiyu na kufanya jumla ya Magari matatu Kwa Mkoa wa Mara na Simiyu.