……..
NA DENIS MLOWE IRINGA
JESHI la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoa wa kimewataka wamiliki wa magari ya shule mbalimbali mkoani hapa kuyapeleka kukaguliwa ili kuweza kuendelea kutoa huduma ya kusafirisha wanafunzi wa shule zao.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa magari 39 yaliyojitokeza katika siku ya kwanza ya ukaguzi , Kamishna msaidizi Meloi Buzema ambaye ni Mkuu wa Oparesheni na Mafunzo ya Kipolisi mkoa wa Iringa alisema watumiaji wa magari yanayotumika kubeba wanafunzi kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuhakikisha magari hayo yamekaguliwa na kitengo hicho kabla ya kufunguliwa kwa shule hapo mwakani.
Alisema kuwa magari hayo yanayobeba wanafunzi wa shule za chekechea, msingi na Sekondari yanatakiwa kuwa katika hali ya ubora ili kuepuka madhara yanayoweza sababisha madhara yakiwa barabarani.
Aliongeza kuwa zoezi hilo la lazima kwa magari litafanyika kwa siku mbili ambapo wamiliki ambao hawajaleta magari hayo walete yakaguliwe kwa mujibu wa sheria kwamba gari inayotembea barabarani iwe na ukamilifu bila kuwa na hitalafu.
Afisa huyo wa jeshi la polisi amesisitiza ”Na tutarudia kuyakagua magari yale ambayo yameonekana na makosa tuone kama yako tayari kwa ajili ya kubeba watoto tarehe za kufungua shule ili yaweze kutoa huduma hiyo na yasipokamilisha hilo tutayaondolea namba hadi yatimize vigezo.”Alisema
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi Iringa, Buzema aliwataka wamiliki kusimamia na kuangalia wasije usije wakapuuza ba kisha wasione kwamba Polisi wanawasumbua hii ukaguzi kwa ajili ya usalama wa watoto wetu.
Kwa upande wake Mkuu kitengo cha usalama barabarani Mkoa wa Iringa, Glory Mtui ametaja changamoto zilizobainika kupitia ukaguzi huo uliofanyika ikiwemo baadhi ya magari ni uchakavu wa matairi, mifumo wa usukani ,kutokuwa na mikanda ya abiria pamoja na ubovu kwa baadhi ya viti na gari kuwa chakavu.
Amesema ukaguzi wa magari katika Mkoa wa Iringa utakuwa unafanyika baada ya miezi mitatu ambapo wiki hii jumla ya magari ya shule 39 yamekaguliwa na kati ya hayo 15 yamebainika na kasoro na kupewa maelekezo nini cha kufanya na kurudisha kukaguliwa.
Aidha alisema wataendelea kutoa elimu kwa wamiliki wa shule zenye magari kuhusu kuwa na vyombo kamilifu vya usafirishaji na kutoa wito kwa shule zote zenye magari ambao hawajitokeza kukagua wafanye hivyo kwani hawataachwa
Naye mmoja ya wamiliki wa shule zilizopoeleka magari kukaguliwa na Mkurugenzi wa Shule ya watoto ya GoodVictory , Emmanuel Nyingi alilishukuru jeshi la polisi kitengo aibu cha Usalama barabarani kwa zoezi hilo na kutoa wito kwa jeshi kulifanya endelevu ili kuwe na usalama wa watoto wetu wanaposafirishwa
Alisema kuwa zoezi la ukaguzi wa magari liwe endelevu ambapo amewataka madereva wanaoendesha magari mabovu kutoa taarifa sehemu husika ili wamiliki waweze kuchukua hatua za matengenezo
Nyingi alisema lengo la ukaguzi huo ni kuimarisha usalama hasa kwa wanafunzi barabarani kuepusha ajari zinazochangiwa na ubovu wa magari pamoja na uzembe wa madereva