Mratibu wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) upande Kuanzisha na kuhuhisha Mitaala ya Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Joseph Sungau akizungumza jambo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengewa uwezo Wahadhiri wa chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kuhusu namna ya kuthibiti Ubora katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufundishaji pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho yaliyofanyika leo Disemba 10, 2024 jijini Dar es Salaan (PICHA NA NOEL RUKANUGA)
Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Kitengo cha Uthibiti Ubora Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Lawrencia Mushi akizungumza jambo katika mafunzo ya kuwajengewa uwezo Wahadhiri wa chuo hicho Ndaki ya Dar es Salaam kuhusu namna ya kuthibiti Ubora katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufundishaji pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa yaliyofanyika leo Disemba 10, 2024 jijini Dar es Salaam.
Washirikiwa wa mafunzo Wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja.
……..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wamejengewa uwezo wa namna ya kuthibiti Ubora kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) jambo ambalo litasaidia kujenga utamaduni wa kuboresha ubora na utendaji hususani katika ufundishaji pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.
Akizungumza leo Disemba 10, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kuhusu uthibiti ubora kupitia Mradi Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), Mratibu wa Mradi wa HEET upande Kuanzisha na kuhuhisha Mitaala ya Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Joseph Sungau, amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kujenga utamaduni wa kuboresha ubora wa vitu vyote vinavyomilikiwa na Chuo hicho ikiwemo ufundishaji.
Dkt. Sungau amesema kuwa mafunzo hayo yanakwenda kuongeza ufanisi kwa wahadhiri pamoja na wafanyakazi katika kuhakikisha wanakuwa na ubora katika utendaji pamoja na kuzingatia kila mmoja ana wajibika katika nafasi yake.
“Tunaendelea kuboresha huduma zetu, warsha hii itawajengea utamaduni mzuri, hivyo tutazalisha wahitimu wanaohitajika sokoni pamoja na kutoa huduma inayoendana na vigezo kulingana na mahitaji ya wateja” amesema Dkt. Sungau.
Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Kitengo cha Uthibiti Ubora Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Lawrencia Mushi, amesema kuwa mafunzo hayo ni muendelezo wa kuwajengea uwezo wanataaluma pamoja na wafanyakazi waendeshaji ili kuongeza ufanisi katika maeneo ya kazi.
Dkt. Mushi amesema kuwa kutokana changamoo nyingi zinazojitokeza katika soko la ajira pamoja na utekelezaji wa majukumu mbalimbali ikiwemo namna ya kuifikia jamii, utafiti na ufundishaji umebaini kuna baadhi ya maeneo kuna mapungufu.
“Tunataka kuwa na bidhaa bora hasa wanafunzi wanaomaliza katika chuo chetu waweze kuwa sifa zinazoitajika katika soko la ajira ndani na nje ya nchi pamoja na kuishi katika viwango vinavyotakiwa” amesema Dkt. Mushi.
Kaimu Naibu Rais wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coletha Komba, amesema kuwa mafunzo hayo yanakwenda kuwasaidia kuongeza ubora katika utendaji kazi ikiwemo uzalisha wahitimu wenye sifa pamoja na kuandaa ripoti zenye ubora.
“Mafunzo yanatukumbusha na kujifunza vitu vipya kwani mambo yanabadilika kila wakati, ni mafunzo rafiki kwa maendeleo ya chuo na sisi binafsi, tutaendelea kufanya kazi vizuri, hivyo jamii wategemee mambo mazuri kutoka kwetu” amesema Dkt. Komba.
Mafunzo ya uthibiti ubora kupitia Mradi wa HEET yatafanyika kwa siku mbili kuanzia Disemba 10- 11, 2024 katika Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam ambapo Wahadhiri na Wafanyakazi Waendeshaji watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ya kitaaluma yenye lengo ya kuongeza ufanisi katika utendaji.
Karibu Mzumbe,Tujifunze kwa maendeleo ya watu.