Wenyeji CS Constantine wametoka nyuma na kushinda 2- 1 dhidi ya Simba SC katika mchezo wa kundi A kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa leo Disemba 8, 2024 katika Uwanja wa Mohamed – Hamlaoui mjini Constantine, Algeria.
Benki na Nahodha Hussein ‘Tshabalala’ alianza kuifungia Simba SC dakika ya 24 kwa shuti la mbali kutoka upande wa kushoto wa uwanja bao ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Dakika moja baada ya kuanza kipindi cha pili beki Abdulrazack Mohamed akijaribu kuokoa shambulizi la kona alijifunga akijaribu kuokoa shambulizi la kona na kuipatai CS Constantine bao la kusawazisha.
Kabla ya mshambuliaji Brahim Dib kuwafungia wenyeji bao la ushindi dakika ya 50 ya mchezo huo.