Wenyeji MC Alger wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2- 0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa kundi A ligi ya Mabigwa Afrika usiku wa Jumamosi Disemba 7, 2024 uliochezwa katika Uwanja wa Julai 5, 1962 jijini Algiers Nchini Algeria.
Mabao ya MC Alger yamefungwa na Benki Ayoub Abdellaoui dakika ya 64 na mshambuliaji Soufiane Bayazid dakika ya 90 + 5 katika mchezo wa kundi A.
Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Yanga ambayo ilianza michuano hiyo vibaya baada ya kukubali kipigo cha mabao 2 -0 na Al Hilal wakiwa Nyumbani katika uwanja wa Benjamini Mkapa.
Mchezo mwengine wa Kundi A utachezwa leo Disemba 8, 2024 ambapo Al Hilal watakuwa wenyeji wa Tp Mazembe katika Uwanja wa Cheikha Ould Boidiya jijini Nouakchott, Mauritania.