Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira Bunda Buwasa Mkoani mara imetambulisha Mradi mpya wa usambazaji maji katika kata ya wariku unaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 ambao utasaidia kuondoa changamoto ya ukosefu wa Maji katika kata hiyo.
Akizungumza Wakati wa kutambulisha Mradi kwa wananchi Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hiyo Ester Gilyoma amesema mradi huo Tayari Mambo yameshanza kupelekwa mabomba katika eneo hilo na inatarajiwa kuanza mwezi huu Disemba na inatarajiwa kukamilika mei 31 2025.
“wananchi wawariku tunaomba mtuamini maana Mradi wetu utakuwa wa miezi Sita natunaamini tutakamilisha kwa wakati kutokana na Serikali kuwekeza nguvu kubwa katika hilo.
Gilyoma aliwataka wakazi wa wariku kuhakikisha wanakuwa walinzi wa miundombinu ya maeneo yao kutokana na kuwepo na historia mbaya ya wizi wa miradi.
Aidha kwa upande wake katibu Tawala Wilaya ya Bunda Salum Mtelela amewaonya wote watakaojihusisha uharibifu wa miundombinu hiyo.