Ujenzi wa jengo la Mikutano la Ofsi za kamisheni ya Bonde la Ziwa victoria linalogharimu kiasi cha shilingi Milioni 3.54 fedha za kimarekan ambazo nitakribani Bilioni 10 za kitanzani limefikia hatua nzuri katika ujenzi wake.
Akizungumzia ujenzi huo Katibu Mkuu wa jumuiya ya Africa mashariki Mheshimiwa Veronica Nduva amesema kwa sasa wanaridhishwa na ujenzi huo ambao umefikia Asilimia 85 na kufikia mwakani ujenzi wa ofisi hizo utakamilika mapema.
” Hii jengo nimmoja ya Miradi inayolenga kuwa na maendeleo endelevu ya jumuiya kuhakikisha siku za usoni tunakuwa na mahala pamikutano na mahala na mawasilisho kuhusu mtengamano wa Africa mashariki unaendeleaje”Alisema Bi.Veronica Nduva katibu Mkuu jumuiya ya Afrika Mashariki.
Veronica amesema kwa bejeti ijayo wamepangiwa bajeti kwaajili ya kuongezewa fedha za ukamilishaji wa jengo hilo ili kuhakikisha linakamilika.