Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), (Katikati), akisaini mikataba minne (4) yenye jumla ya euro milioni 118.8 sawa na takriban shilingi bilioni 323.4 kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwemo Awamu ya Pili ya Mradi wa Nishati-jua wa Kishapu Mkoani Shinyanga pamoja na uendelezaji wa misitu na utunzaji wa Hifadhi ya Misitu ya Mikoko, zilizotolewa na Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo (AFD), Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Axel-David Guuillon na kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Celine Robert.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), (Katikati), akibadilishana na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Celine Robert, moja kati ya Hati Nne za Mikataba yenye jumla ya euro milioni 118.8 sawa na takriban shilingi bilioni 323.4 zilizotolewa na AFD, kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwemo Awamu ya Pili ya Mradi wa Nishati-jua wa Kishapu Mkoani Shinyanga pamoja na uendelezaji wa misitu na utunzaji wa Hifadhi ya Misitu ya Mikoko, Anayeshuhudi kulia ni Naibu Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Axel-David Guuillon, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), Katikati), Naibu Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Axel-David Guuillon (kulia) na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Celine Robert, wakionesha Hati za Mikataba yenye jumla ya euro milioni 118.8 sawa na takriban shilingi bilioni 323.4 zilizotolewa na AFD, kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwemo Awamu ya Pili ya Mradi wa Nishati-jua wa Kishapu Mkoani Shinyanga pamoja na uendelezaji wa misitu na utunzaji wa Hifadhi ya Misitu ya Mikoko, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), (Katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania na Ufaransa baada ya kuia Saini Hati za Mikataba Minne (4) yenye jumla ya euro milioni 118.8, sawa na takriban shilingi bilioni 323.4 zilizotolewa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwemo Awamu ya Pili ya Mradi wa Nishati-jua wa Kishapu Mkoani Shinyanga pamoja na uendelezaji wa misitu na utunzaji wa Hifadhi ya Misitu ya Mikoko. kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Danstun Kitandula, kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, wa pili kulia ni Naibu Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Axel-David Guuillon na wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Celine Robert na Maafisa wengine wa Serikali kutoka Tanzania na Ufaransa. Tukio hilo limefanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WF, Dar es Salaam)
………..
Na Farida Ramadhani,WF, Dar es Salaam
Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo La Ufaransa (AFD) wamesaini mikataba minne (4) yenye jumla ya euro milioni 118.8 sawa na takriben shilingi bilioni 323.4 kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwemo Awamu ya Pili ya mradi wa nishati jua wa Kishapu Mkoani Shinyanga, pamoja na uendelezaji wa misitu na utunzaji wa hifadhi ya misitu ya mikoko.
Hafla ya utiaji saini wa Mikataba hiyo imefanyika jijini Dar es Salam kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kwa upande wa Serikali na Naibu Balozi wa Ufaransa nhini Tanzania, Mhe. Axel-David Guuillon pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Celine Robert.
Akizungumza baada ya kusaini Mikataba hiyo, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema katika Mikataba hiyo iliyosainiwa euro milioni 75.9 ni kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Nishati ya jua unaotekelezwa Kishapu Mkoani Shinyanga.
Alisema kuwa mradi huo utazalisha Megawati 150 ambapo Awamu ya Kwanza upo katika hatua za utekelezaji na unatarajiwa kuzalisha Megawati 50 na Awamu ya Pili ambayo mkataba wake umesainiwa inatarajiwa kuzalisha Megawati 100 na kufanya jumla ya Megawati zitakazozalishwa kuwa 150.
‘’ Kuingiza Megawati 150 kwenye gridi ya Taifa, kutapunguza utegemezi wa nishati ya nguvu za maji ambayo inaathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Mradi huu utaongeza upatikanaji wa nishati ya uhakika katika Mkoa wa Shinyanga ambao una umuhimu wa kimkakati wa kiuchumi na kijamii kutokana na kuwepo kwa shuhguli kubwa na ndogondogo za uchimbaji madini” alibainisha Mhe. Dkt. Nchemba.
Alisema Mkataba wa pili wa Euro milioni 39.9 ni kwa ajili ya uendelezaji wa mashamba ya misitu na utunzaji wa hifadhi ya mikoko ili kuongeza wigo wa upandaji miti, kuboresha ubora na wingi wa mbegu za miti na kuboresha usimamizi wa mbegu hizo.
Alisema mradi huo utaimarisha vituo vya kukusanya mbegu za miti na kuanzisha vitalu vya kisasa vya miti ikiwa ni pamoja na kutaboresha utunzaji wa hifadhi ya misitu ya mikoko, kuboresha uhifadhi wa uhasilia wa mazingira na kuchangia kuinua utalii na kuboresha Maisha ya jamii.
Dkt. Nchemba alisema mikataba ya euro milioni 2 ni kwa ajili ya utunzaji wa hifadhi ya mikoko na euro milioni 1 ni kwa ajili ya kufadhili Mpangokazi wa Jinsia unaotekelezwa na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO), chini ya mradi wa uendelezaji wa nishati ya Jua.
“Huu ni mwendelezo wa ushirikiano wetu mzuri ambao umeshuhudiwa kwa kuwepo kwa miradi mbalimbali ambayo inafadhiliwa kwa mikopo nafuu kutoka Serikali ya Ufaransa kupitia AFD”, alisema Mhe. Dkt. Nchemba.
Alisema kuwa Serikali ya Ufaransa kupitia AFD imefadhili miradi mbalimbali kupitia mikopo nafuu katika sekta za Nishati, Maji, Usafirishaji na Kilimo ambayo mingine inaendelea na mingine imekamilika.
Naye Kaimu Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Axel-David Guuillon alisema miradi itakayotekelezwa kupitia mikataba hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi kwa kuwa itasaidia kupunguza gharama za kuagiza mafuta pamoja na kuhifadhi mazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi. Celine Robert, alisema kuwa mikataba hiyo ni mwendelezo wa uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Shirika hilo.
Alisema mkataba wa kuendeleza misitu nchini utaiwezesha Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kujumuisha ukuaji wa uchumi, ushirikishwaji wa jamii na utunzaji endelevu wa mazingira.
Bi. Robert alisema mkataba wa Awamu ya Pili ya mradi wa nishati ya jua Kishapu Mkoani Shinyanga, utaiwezesha nchi kukabiliana na changamoto za umeme kwa kuwa Tanzania itakuwa na vyanzo tofauti tofauti vya umeme.
“Mabadiliko ya hali ya hewa yapo na yanaathari nyingi siku za usoni, mradi huu wa umeme utaiwezesha Tanzania kukabiliana na tatizo la umeme hususani yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na kutunza mazingira” alisema. Bi. Robert.
Kwa upande wa Manaibu Mawaziri wa Sekta ambazo zitatekeleza miradi hiyo walisema watasimamia kikamilifu miradi hiyo ili kuhakikisha inafikia malengo kusudiwa ambapo Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga alisema mkataba wa Awamu ya Pili ya mradi wa nishati ya jua Kishapu Mkoani Shinyanga ni mradi muhimu ambao unaenda kuchagiza miradi mingine ambayo inazalisha nishati jadidifu ambazo zinapunguza athari za mazingira.
Naye Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula, alisema fedha hizo zilizosainiwa katika mikataba hiyo zitatumika kupanda miti na kusimamia misitu ya mikoko.
Alisema mikataba hiyo itaiwezesha nchi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuongeza uwezo wa kuvuna mazao yanayotokana na misitu