Mshauri wa Ulinzi na Haki ya Mtoto kutoka Shirika la Save The Children Wakili Barnabas Kaniki akiwaelimisha wanafunzi kuepukana na ukatili wa kijinsia katika kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika shule ya Sekondari ya wasichana Kisutu pamoja na Sekondari ya Zanaki jijini Dar es salaam leo Dec 3n2024 kwa utaribu na Shirika la Save The Children
Askari mpelelezi wa Makosa ya Jinai kutoka dawati la jinsia na watoto Kanda Maalum ya Dar es salaam Eva Simon Mbesere akiwaelimisha wanafunzi kuepukana na ukatili wa kijinsia katika kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika shule ya Sekondari ya wasichana Kisutu pamoja na Sekondari ya Zanaki jijini Dar es salaam leo Dec 3n2024 kwa utaribu na Shirika la Save The Children
Afisa Ustawi wa Jamii na Mratibu wa Dawati la familia na watoto Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Christon Cletus akiwaelimisha wanafunzi kuepukana na ukatili wa kijinsia katika kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika shule ya Sekondari ya wasichana Kisutu pamoja na Sekondari ya Zanaki jijini Dar es salaam leo Dec 3n2024 kwa utaribu na Shirika la Save The Children
Baadhi ya wanafunzi ambao wamejengewa uwezo wa namna ya kuepukana na masuala ya ukatili wa kijinsia katika katika kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa utaribu na Shirika la Save The Children.
…………….
NA MUSSA KHALID
Shirika lisilokuwa la kiserikali la Save The Children kwa kushirikiana na Maafisa ustawi kutoka Jeshi la Polisi na Halmashauri wametoa elimu ya masuala ya Ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa Sekondari ya Kisutu na Zanaki jijini Dar es salaam ili waweze kuepukana na vitendo hivyo.
Hayo yamejiri ikiwa ni katika muendelezo wa kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia ambayo huwa inaanza mwezi Novemba 25 mpaka Disemba 10 ya kila mwaka.
Akizungumza katika halfa ya kuwaelimisha wanafunzi katika Shule ya Sekondari Kisutu na Zanaki zilizopo jijini Dar es salaam Mshauri wa Ulinzi na Haki ya Mtoto kutoka Shirika la Save The Children Wakili Barnabas Kaniki amesema wanachokifanya ni Hatua ya Kuzuia vitendo vya ukatilii visitokee kwa kuwaelimisha kufahamu ni namna gani wanaweza kuepukana na vitendo vya ukatili katika jamii yao.
“Hatuna Ukatili mdogo Wala Mkubwa kwani Ukatili ni Ukatili tu hivyo unavyobaini unafanyiwa kitendo chochote cha kikatili hakikisha unatoa taarifa”amesema Kaniki
Kwa upande wake Askari mpelelezi wa Makosa ya Jinai kutoka dawati la jinsia na watoto Kanda Maalum ya Dar es salaam Eva Simon Mbesere amewasisitiza wanafunzi hao kutambua Haki na wajibu ikiwemo kuwa mabalozi kwa wanafunzi wenzao katika kuepukana na vitendo vya ukatili.
“Kwenye Makosa ya shambulio la aibu tunapofanyiwa tuhakikishe hatufumbii vitendo vya namna hiyo Bali tukatae Ili mtu akawajibishwe kwa mujibu wa Sheria”amesema Askari Eva
Naye Afisa Ustawi wa Jamii na Mratibu wa Dawati la familia na watoto Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Christon Cletus amewasisitiza wanafunzi hao kuhakikisha wanatumia namba ya 116 Ili kutoa taarifa za Ukatili ambao wamefanyiwa endapo wanakuwa na hofu.
Baadhi ya wanafunzi kutoka katika shule hizo wamepongeza hatua hiyo ya Shirika ka Save The Children kuwapatiwa elimu namna ya kujilinda na ukatili lakini pia kutoa taarifa kwa wakati sehemu husika pindi wanapokumbana na tukio la ukatili.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Zanaki Damian Balasa ameishauri serikali kufanyika marekebisho sheria kinzani ili kuondoa migongano katika jamii ambazo zimekuwa zikitumia kufanya ukatili.