Mkuu wa Idara ya Kozi Fupi na Shauri za Kitaalamu Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Darlene Mutalemwa akizungumza jambo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa Chuo hicho yaliyofanyika katika Kituo cha Tegeta, Dar es Salaam. (PICHA NA NOEL RUKANUGA)
Makamu wa Rais wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) CPA. Victorious Kamuntu akizungumza jambo wakati akiwajengea uwezo wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Kituo cha Tegeta kuhusu kukabiliana na changamoto ikiwemo kuboresha uwezo wao wakiwa chuo pamoja na kutengeneza mtandao na Taasisi mbalimbali.
Diwani wa Kata ya Yombo Vituka, Fulgence Lwiza akizungumza jambo wakati akiwajengea uwezo wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Kituo cha Tegeta kuhusu kukabiliana na changamoto ikiwemo kutafuta fursa za ajira au kujiajiri wakiwa chuoni.
Mkufunzi Bi. Hawa Lulengo akizungumza jambo wakati akiwajengea uwezo wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Kituo cha Tegeta kuhusu kukabiliana na changamoto ikiwemo kuwa na nidhamu pamoja na kumtegemea Mungu wakati wote.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Bw. Kosta Mashi akizungumza jambo wakati akiwashukuru wakufunzi pamoja na uongozi wa chuo kwa kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Kituo cha Tegeta wakiwa darasani wakifatilia mafunzo ya kujengewa uwezo.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Kituo cha Tegeta wakiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi na uongozi wa chuo baada ya kumalizika kwa mafunzo chuoni hapa.
………………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam imewajengea uwezo wanafunzi wa Chuo hicho kwa ajili ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuwa na sifa ya kuajiriwa na kujiajiri baada ya kumaliza masomo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Kozi Fupi na Shauri za Kitaalamu, Dkt. Darlene Mutalemwa, amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia wanafunzi kufanya vizuri baada ya kumaliza masomo yao.
Amesisitiza muhimu wa kila mwanafunzi kuwa na bidii ya kusoma pamoja na kutumia fursa zilizopo ili kukabiliana na changamoto zilizopo.
Nao wakufunzi wa mafunzo hayo akiwemo Makamu wa Rais wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) CPA. Victorious Kamuntu, amesema kuwa
wakati umefika kwa vijana kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo yao kuwekeza ili kukabiliana na changamoto ya ajira nchini, kwa kuwa Serikali imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji.
CPA. Kamuntu amesema kuwa waajiri wengi wanapenda kuajiri mwanafunzi wenye uwezo wa kufanya kazi kwa uweledi ikiwemo kutumia teknolojia ambazo zitamsaidia katika utendaji wa kazi.
“Waajiri hawaangalii umepata GP ya ngapi, wanafunzi wengi wamesahau mambo ya msingi wanayapaswa kufanya wakiwa chuoni, nawakumbusha wasome kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao” amesema CPA. Kamuntu.
Diwani wa Kata ya Yombo Vituka, Fulgence Lwiza, amesema kuwa vijana wanapitia katika hali ambayo wanapaswa kujitambua na kuwajibika kwa namna moja au nyengine ili waweze kupiga hatua.
Lwiza amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikiwajali wanafunzi hali ambayo imepelekea kutoa elimu bure kuanzia elimu ya awali hadi Sekondari.
“Vijana wanapaswa kuchangamkia fursa zilizopo kuna mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri, ni muda wa vijana kuamka na kuachana na fikra ya lazima waajiriwe baada ya kumaliza masomo yao” amesema Lwiza.
Akizungumza kwa niaba ya Wanafunzi, Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Bw. Kosta Mashi, ameushukuru uongozi wa Chuo kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yanakwenda kuwa msaada katika maisha yao baada ya kumaliza masomo chuoni hapo.
Bw. Mashi amesema kuwa wamefundishwa mambo mengi yenye manufaa katika kuongeza uwezo, huku akiwaasa wanafunzi wenzake kwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo.
Katika mafunzo hayo wanafunzi wamejengewa uwezo na wakufunzi ambao wamewai kusoma katika Chuo hicho ambapo wamefundishwa mada mbalimbali ikiwemo nini wanapaswa kufanya wakiwa Chuo, uwezo wa kukabiliana na mambo ya msingi baada ya kumaliza Chuo, namna ya kuboresha uwezo wao wakiwa Chuo, kuwa na sifa ya kuajiriwa na kujiajiri, kuwa na mtaji wa uaminifu pamoja kutengeneza mtandao na Taasisi mbalimbali